in , , ,

YUKO WAPI MO-IBRAHIM?

Msimu jana alishirikiana na kina Shiza Kichuya, Mzamiru Yasin kuibeba Simba.

Pamoja na uzito wa Simba , ugumu wa njia walizokuwa wanapitia lakini
walifanya kadri wanavyoweza kuibeba Simba.

Simba ambayo ilikuwa bingwa wa kombe la chama cha soka nchini (TFF)

Simba ambayo ilishika nafasi ya pili kwenye ligi kuu ya Tanzania bara
nyuma ya Yanga kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Simba ilikuwa haina safu kali ya ushambuliaji kitu ambacho kilichangia
kwa namna moja au nyingine kuzidiwa na Yanga.

Simba iliwatumia kina Mohammed Ibrahim, Shiza Kichuya na wengine
kuhakikisha wanapata magoli.

Kiasi kwamba wachezaji hawa walifanikiwa kushika mioyo ya mashabiki.

Ilikuwa furaha kwa mashabiki kumuona Mohammed Ibrahim akiwa kwenye
orodha ya wachezaji watakaoanza kwenye mechi husika kwa sababu walijua
kuna vitu vingi watapata kutoka kwake.

Uwezo wake wa kumiliki mpira bila kupoteza kilikuwa kitu cha msaada
kwa timu kwa sababu kiliihakikishia timu iweze kumiliki mpira ndani ya
mchezo husika.

Hakuwa mshambuliaji halisi wa katikati lakini magoli yake
yalifanikisha Simba kupata alama tatu muhimu.

Nyimbo yake ilikolea zaidi kipindi alipokuwa anatengeneza magoli
kwenye mchezo husika

Kitu ambacho kilimfanya awe mchezaji muhimu na nguzo kwenye kikosi cha
mwalimu Joseph Omog.

Msimu jana ulipita na nyakati za furaha kwa Mohamed Ibrahimu, lakini
msimu huu zimekuja na nyakati ngumu sana kwake.

Nyakati ambazo zinamfanya kuwa mchezaji ambaye hajapata mechi nyingi
msimu huu kwa sababu mbalimbali kama majeraha na kutokuwa chagua la
kocha.

Siyo jambo la kushangaza kutokuona jina lake kwenye kikosi cha Simba msimu huu

Maisha yamebadilika kwake, kimbuga kikali kimeelekea upande wake,
anahitaji nguvu kubwa kukabiliana na kimbuga hicho.

Nguvu ambayo itasaidia kuokoa kipaji chake, kipaji ambacho wengi
walitamani kukiona kikifika mbali na kusaidia Taifa kwa ujumla.

Mwanga taratibu unaanza kufifia na kulikaribisha giza katika maisha
yake ya mpira.

Anahitajika mtu wa kumwekea mwanga ili aweze kuona ni wapi anapotakiwa
kwenda ili afike alipokuwa anapatamani siku zote.

Najua anapitia nyakati ngumu, nyakati ambazo bila kukaa na mtu wa
karibu wa kumshauri vizuri kuna hatari kubwa ya ƙkumpoteza

Anatakiwa kupokea hali halisi anayoipitia kwa sasa, aambiwe ni kawaida
kwa mwanadamu kupitia nyakati ngumu kwa sababu maisha siku zote ili
yakamilike yanahitaji pande zote mbili ( upande wa furaha na huzuni)

Pande hizo mwanadamu kaumbiwa, na ni lazima mwanadamu azipitie lakini
kinachowatofautisha wengi ni uimara wa kupita katika nyakati ngumu.

Hakuna kipindi ambacho Mohamed Ibrahim anatakiwa kuwa imara kama kipindi hiki.

Anatakiwa kuwa na nguvu za ziada na mawazo chanya katika akili yake
yatakayomwezesha ajijenge yeye kama yeye.

Mawazo chanya ambayo yatampa imani kesho imeumbwa kwa akili yake na
asichoke kuisubiri kesho yake.

Naamini kwenye kipaji chake , naamini anauwezo mkubwa wa kurudi sehemu
ambayo tutamsifu na kumwandika sana kwa kiwango chake bora.

Roho ya kukata tamaa haitakiwi kuwepo na kutawala akili yake, yeye ni
dhahabu inayopita kwenye moto kwa sasa, thamani yake ni kubwa mno siku
moto huo utakapozima

Anatakiwa kuvumilia kila kitu kibaya kinachokuja kwake, hakuna baya
lisilo na faida. Mabaya humfanya binadamu awe imara zaidi.

Huwezi kuwa imara bila kupitia nyakati ngumu katika maisha yako. Hili
ni suala la muda tu, aupe nafasi muda utatoa majibu sahihi kuhusu
maisha yake ya mpira.

Sehemu ambayo ndiyo anaitegemea katika maisha yake.

Huu ndiyo wakati ambao masikio yake yanahitaji pamba, na kukimbia
kuelekea mbele bila kumsikiliza mtu cha muhimu ajue ni wapi amepanga
kwenda.

Afanye mazoezi kwa bidii, ajitume zaidi. Ajitunze vizuri kuanzia
kwenye mlo mpaka muda wa kupumzika, na kila anapoamka awe na hasira ya
kufika juu kupitia mazoezi ya timu na mazoezi yake binafsi, kwa
kufanya hivo kesho itakuwa yake na ataimiliki yeye pekee kwa uweza wa
MUNGU

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

MIKONO YA KABWILI INAPINGANA NA HUKUMU YETU KWAKE

Tanzania Sports

Man City vs Chelsea