West Ham nje Europa

 

*Southampton wasonga mbele

 

West Ham wa England wametupwa nje ya Ligi ya Europa mapema baada ya kuchapwa 2-1 na timu ya Romania, Astra Giurgiu kwenye mechi ya mkondo wa tatu wa kufuzu.

 

Kwa uwiano West Ham wamefungwa 4-3 baada ya kwenye mchezo wa kwanza kuchezea uongozi wao wa mabao mawili kwa bila.

 

Kichapo hicho kimehitimisha kampeni iliyokuwa ikifanywa na kocha mpya, Slaven Bilic. West Ham walifuzu kwa sababu ya kuwa moja ya timu zenye nidhamu zaidi.

 

Katika mechi nyingine, Southampton wamefanikiwa kuvuka hatua kwa mabao ya Graziano Pelle na Sadio Mane dhidi ya Vitesse Arnhem.

 

Saints walikuwa wakicheza kwa mara ya kwanza tangu walipocheza kwenye mechi za Uefa 2003 ambapo walifika hatua za makundi.

Comments