in , , ,

Wanasoka wanavyojihisi juu ya mishahara yao

Mesut Özil

MIAKA 20 iliyopita, Deloitte and Touche walitoa taarifa ya pamoja wakionya juu ya ongezeko kubwa la gharama kwenye Ligi Kuu ya England (EPL).

Theluthi ya klabu zilikuwa zikilipa asilimia 50 ya mapato yao ya mwaka – kwa ajili ya mishahara ya wanasoka wao.

Chelsea walitokea kuwa watumiaji wakubwa zaidi, ambapo katika msimu wa 1997/98 walilipa mishahara ya jumla ya pauni milioni 27. Manchester United walikuwa wa pili kwa kulipa £26.9m; Liverpool wa tatu (£24 m).

Klabu mbili za chini kabisa kwenye ligi hii kubwa, kwa maana ya malipo ya mishahara, zilikuwa
Wimbledon waliolipa pauni milioni tisa na Southampton wakajikamua pauni milioni saba kwa ajili ya mishahara ya wachezaji wao.

Deloitte and Touche walikuwa sahihi. Walikuwa wametilia maanani athari za ‘Bosman Ruling’ miaka mitatu kabla ya hapo, lakini pia wakatazama uwekezaji uliokuwa ukifanywa na Sky kwenye kutangaza mechi ili kulinda kile ambacho kingefuata.

Ndani ya miezi 12 iliyofuata, watangazaji walizidi kuonesha kuwa na maslahi kwenye michezo, ambapo Sky wakawa na Chelsea, Leeds United na Manchester United, huku NTL wakiwaendea Newcastle United and Aston Villa.

Leo hii EPL imesimama kama msimu, kwa sababu ya janga la homa kali ya mapafu, Covid-19 inayosababishwa na virusi vya Corona. Imeua maelfu ya watu na virusi vimekuwa vikisambaa kwa kasi katika mabara mbalimbali kiasi cha ligi karibu zote kusitishwa.

Klabu sasa zinagugumia, kwa sababu ya athari za kiuchumi – zikiwa haziingizi kima kilichotarajiwa ambacho kingetumika kwa ajili ya kuwalipa wachezaji lakini pia gharama nyingine kubwa.

Kuweka viwango vikubwa vya mishahara pasipo kuwa na uhakika wa kipato ni tatizo hilo hilo waliloliona wataalamu hao wa uhasibu na ukaguzi wa hesabu. Lakini pia janga limekuja wakati ambapo klabu zinataka kufanya usajili. Man United wameshasema tayari kwamba hapatakuwapo usajili wa kishindo – hakuna fedha.

Zipo klabu ambazo tayari zinajielekeza kwenye kusajili wachezaji kadhaa watakaokuwa huru kipindi cha kiangazi na wale wa Januari kwenye dirisha dogo mwakani, kwani klabu wameyumba mno kiuchumi. Ni vyema matumizi ya fedha yakawa ya kiasi badala ya kutapanya.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Soka itachukua muda kurejea kawaida

Tanzania Sports

Covid-19 imembadili Boris Johnson