in

Waarabu wagonga mwamba kununua Newcastle

Mike Ashley

DILI la kuinunua timu ya Newcastle United la pauni milioni 300 limeota mbawa baada ya waarabu wa PIF (Public Investment Fund) kutoka Saudi Arabia kujitoa kwenye mchakato huo.

Taarifa iliyochapishwa na gazeti la Guardian imesema kuwa waendeshji wa Ligi Kuu England walitonywa kuwa ofa ya asilimia 80 kuinunua klabu hiyo ingetoka kwa Mfuko wa Umma wa Uwekezaji (Public Investment Fund) ambayo ni moja ya mali ya serikali ya Saudi Arabia.

Hoja hiyo imetumika kuingilia kati mpango wa kuinunua Newcastle, kwa sababu serikali ya Saudi Arabia imekuwa ikiweka vikwazo dhidi ya waendeshaji wa Ligi Kuu England kuifungulia mashtaka beoutQ kwa kuonyesha  mechi za Ligi hiyo kinyume cha sheria.

Mwanzoni mwa mwezi Julai PIF walipewa ofay a kuboresha ofa yao, lakini imebainika kuwa mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman ambaye pia ni mwenyekiti wa PIF walishindwa kufanya maboresho yoyote.

Tanzania Sports
Mike Ashley, na mdau wa Newcastle Utd

Taarifa kutoka kwa wasimamizi wa Ligi Kuu England zimesema PIF walishindwa kuthibitisha kwa Shirika la Biashara Duniani (WTO) kuwa beoutQ inatoa huduma kama kampuni binafsi au inamilikiwa na serikali ya Saudi Arabia.

Aidha, imedaiwa kuwa serikali ya Saudi Arabia imekuwa ikikuka sheria za Hatimiliki kwa kushindwa kudhibiti kampuni ya beoutQ inayoonesha mechi za ligi bila idhini, licha ya kudai uamuzi wa WTO unawapa ushindi Saudia.

Huu inadhihirisha kuwa Ligi Kuu imewasilisha ushahidi moja kwa moja kwa WTO juu ya uharamia wa Saudi Arabia. Mwezi uliopita Ofisa Mtendaji Mkuu wa Ligi kuu, Riachard Masters aliliambia bunge kuwa wameitaka Saudi Arabia kutoa majibu juu ya hakimiliki za kampuni za michezo kulinda haki zao dhidi ya uharamia. 

Mpango wa kuinunua Newcastle ulikubaliwa mwezi Machi mwaka huu na mmiliki wake Mike Ashley baada ya kuwekwa wazi timu hiyo inahitaji mmiliki mpya, hali ambayo iliibua vita vya umiliki ambavyo vimekuwa vikiendeshwa kati ya nchi mbili za Saudi Arabia na Qatar kwa kipindi cha miaka mitatu. Nchi hizo zimekuwa zikipambana kumiliki klabu za Ligi Kuu England ambapo Qatar kupitia Tynesiders ilikuwa na nia ya kutimiza ndoto za kuibua klabu tajiri England.

Hata hivyo taarifa zinasema mwezi Aprili Bodi ya Ligi Kuu iliwatonya PIF kuwa dili la kuinunua Newcastle lingeidhinishwa kwa vile hapakuwa na dalili zozote za vikwazo, lakini matatizo ya Saudi Arabia yaliingizwa kwenye Bodi na kuibua mtazamo mpya kutaka serikali ya Saudi Arabia ijitoe katika umiliki wa PIF, na kwamba pawepo utengano wa kisheria kati ya PIF na serikali.

Kama ambavyo mashabiki Newcastle wanavyohaha kumkubali Mike Ashley alyepoteza umaarufu klabuni hapo, ndivyo ilivyotokea kwa Amanda Staveley ambaye aliongoza mipango ya kuimiliki timu hiyo kwa ushirikiano kupitia PCP Capital Partners alimwaga machozi kuwa Richard Masters amepata shinikizo kutoka kwa klabu pinzani, hasa Liverpool na Tottenham zinazopinga kununuliwa Newcastle United.

“Tumesikitishwa sana. Ukweli tunaweza kuilaumu Bodi ya Ligi Kuu. Wao walikuwa na nafasi, wanasema hatujatoa majibu ya maswali na sisi tumefanya hivyo. Lakini klabu zingine za Ligi Kuu zimekataa mpango huo kufanyika alisema Staveley  na kuongeza kuwa “uharamia halikuwa tatizo lakini tumejitahidi kutatua tulivyoweza. Bodi ya Ligi Kuu imejaribu kujenga hoja kuwa serikali ya Saudi Arabia ndio mkurugenzi. Wakati PIF ilikubali kuwa mkurugenzi.

Henry Mauriss, mfanyabiashara wa Marekani ameripotiwa kutoa ofay a pauni milioni 350 kwa Mike Ashley ili kununua Newcastle lakini inadaiwa alipuuzwa.

Mashirika ya haki za binadamu yamekuwa yakishanikiza Bodi ya Ligi Kuu kuifungia milango PIF kununua Newcastle kwa kile ilichodai ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Saudi Arabia hususani kuuawa kwa mwandishi Jamal Khashoggi.

“Ukweli ni kwamba kufeli kwa mpango wa kununua Newcastle utaonekana kama dalili ya watetezi wa haki za binadamu nchini Saudi Areabia kuwa hoja zao hazijapuuzwa,” alisema Peter Frankental  wa shirika la Amnesty International Uingereza.

“maelfu ya watetezi wa haki za binadamu nchini Saudi Arabia wamefungwa magerezani, na waandishi wa habari wamekumbwa na misukosuko na wengne kuuawa na mawakala wa ujasusi wa Saudi Arabia kwa miaka miwili iliyopita. Ninavyotazama mbele, kunahitajika mabadiliko ya utawala kuhakikisha wamiliki na wakurugenzi wa timu za Ligi Kuu wanapimwa kwa vigezo vya haki za binadamu kwa wote wanaotaka kununua timu, bila kujali mnunuzi ni serikali au mwakilishi wa serikali,”

Andrew Smith mwanaharakati dhidi ya biashara ya silaha amesema, “hayo ni matokeo sahihi kwa sababu mbovu. Makubaliano hayakupaswa kuchukua hatua zozote. Historia na tabia ya utawala wa Saudi Arabia vilitosha kutumika kuzuia mpango wa kuinunua Newcastle,”

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Gianni Infantino

Pingu zamnyemelea’ Rais wa FIFA

Arsenal

Ni Arsenal tena……