in

Vigogo vya soka Tanzania vyawachefua mashabiki , wanachama wake

TIMU za soka za Simba na Yanga za  Dar es Salaam zimeuanza vibaya mwaka 2012 kwa kupata vipigo kwenye mechi za kuwania Kombe la Mapinduzi Zanzibar mwaka huu  jambo ambalo limezitonesha kidonda timu hizo cha kufungwa kwenye mechi tofauti za kirafiki zilizofanyika wakati wa kumaliza mwaka 2011.

Yanga ndiyo ilikuwa ya kwanza ambapo Jumatatu usiku wa kuamkia Jumanne wiki hii ilicharazwa goli 1-0 na timu  changa ya Mafunzo ya Zanzibar ukilinganisha na ukongwe wa Yanga.

Michuano ya Kombe la Mapinduzi inashirikisha timu tatu kutoka Tanzania Bara na zingine tatu za Tanzania Zanzibar.

Kipigo hicho kwa Yanga kilitokea wakati ikikumbuka kufungwa mwishoni mwa mwaka jana magoli 2-0 na timu ya Azam FC inayojiandaa kutawala Tanzania kisoka na kiuendeshaji kutokana na kuwa ya kwanza nchini kuwa na uwanja wa kisasa na maeneo mbalimbali ya kufanyia mazoezi.

Kwa upande wa Simba SC  ambayo mwishoni mwa mwaka jana ilichabangwa magoli 3-2 na timy ya watengeneza Sukari Mtibwa ya Morogoro, usiku wa kuamkia leo Jumatano imekiona cha moto baada ya kuchapwa magoli 2-1 na timu ya Jamhuri kutoka Pemba.

Pigo hilo limekuja baada ya kushuhudia mkongwe mwenzake alipoburuzwa kwenye uwanja huohuo wa Amani Zanzibar kuwani kombe la Mapinduzi ambalo kwa sasa linashikiliwa na Simba.

Kufungwa kwa timu hizo kumewachefua mashabiki wake hususan walioko Tanzania bara ambao kwa jana walishindwa kutambiana kutokana na timu zao kugaragazwa kwenye mashindano hayo wakati zikiwa kwenye maandalizi makubwa ya Ligi Kuu ya VODACOM na pia zinajiandaa na michuano ya Afrika.

Yanga ambayo ni bingwa Tanzania, kwa sasa inajiandaa kumenyana na Zamalek ya Misri katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika  wakati nayo Simba inajiandaa kucheza na Kinyovu ya Rwanda katika mechi za Kombe la Shirikisho  zinazoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Lakini pia vipigo hivyo kwa klabu kongwe za Bara, vinaashiria wazi kwamba soka la Zanzibar linazidi kukua kwani mpaka sasa ni timu ya Azam FC kutoka Bara ambayo imepata ushindi  kwa kuifunga magoli 3-1 timu ya Kikwajuni Zanzibar.

Mechi zinazotarajiwa kufanyika baadaye kuanzia leo jioni ni  za Yanga kwa kucheza na Kikwajuni, Azam  na Mafunzo wakati Simba nayo imebakiza mechi dhidi ya Miembeni na KMKM.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Yanga yatakiwa kuacha nyodo Zanzibar

Wadau ndani ya BBC Bush House Club……