in , ,

VIATU VYA SCOTT VIMEFICHA PESA ZA POGBA

Muda huu kelele za pesa hazisikiki kwa kiasi ƙkikubwa kama ilivyokuwa
awali, mategemeo yetu yalikuwa makubwa sana baada ya kuamua kutumia
pesa nyingi kununua pasi za mwisho, magoli na uwezo wa kukaba na
kushambulia.

Tuliamini pesa zimeleta mtu ambaye angekuwa na uwezo wa kusimama na
kuonekana kama nembo kubwa ya klabu.

Kila jicho ambalo lilikuwa linatazama uwanja wa Old Trafford lilianza
kuona kwa mbali Paul Pogba kama ndiye nembo kubwa ijayo ya timu

Pengine umri wake ulikuwa unamruhusu kujenga nembo imara kwenye timu
ya Manchester United, na pengine uwezo wake mkubwa aliouonesha katika
timu ya Juventus kabla hajaja Manchester United ndiyo ulitia matumaini
makubwa kuwa Paul Pogba ndiye mfalme ajaye ndani ya kikosi cha
Mnachester United.

Tena alikuja wakati mzuri kwake, wakati ambao milango ya Old Trafford
ilikuwa tayari kufunguka kwa ajili ya kuweka njia ya kutokea kwa Wayne
Rooney, njia ambayo aliitumia Paul Pogba kuingia.

Lilikuwa jambo zuri na ilikuwa vyepesi kwake kuweka jina lake ndani ya
mioyo ya mashabiki wa Manchester United kwa sababu Mfalme Wayne Rooney
alikuwa anamaliza muda wake wa Utawala pale Manchester United

Mioyo ya wengi ilitamani mtawala ajaye angekuwa Paul Pogba kwa sababu
ya pesa zilizotumika kumleta pale Old Trafford, pesa ambazo zilikuwa
deni kubwa.

Msimu wa pili sasa huu unaelekea kuisha tangu pesa zimfanye Paul Pogba
akanyage nyasi za viwanja vya Old Trafford, maendeleo yake
yanakatisha tamaa mpaka sasa.

Wengi wameanza kupoteza imani na tumaini walilokuwa nalo kipindi
ambacho Paul Pogba alipokuwa anakuja katika timu ya Manchester United.

Matumaini ya kuona Paul Pogba akifunga magoli ambayo yangeisaidia timu
kupata mafanikio makubwa yameanza kupotea taratibu.

Hata imani ya wengi ya kutamani kuona Manchester United ikipata
mafanikio makubwa kupitia nguvu na kivuli cha Paul Pogba imeanza
kupotea.

Watu wengi wanatamani nyakati zile zilizokuwa na majira ya Juventus
ndani ya maisha ya Paul Pogba zijirudie lakini ndivyo hivo upepo
umekuwa mkali sana kwa Paul Pogba.

Umekuwa upepo wenye nguvu kubwa sana, tena kibaya zaidi ni upepo wa
mawe na unavuma kuelekea kwenye uso wa Paul Pogba, muda huu ana kazi
moja tu kubwa nayo ni kutumia mikono yake kujikinga uso wake dhidi ya
upepo.

Hana kazi nyingine ya ziada kitu ambacho kimesababisha hata kocha wa
Manchester United kutoendelea kumwamini kwa muda huu na imani yake
kuielekeza kwa kijana mdogo sana Scott McTominay.

Viatu vyake vinaonekana vimebeba mahitaji muhimu anayoyataka Jose
Mourinho. Ndiyo maana ikawa virahisi kwa Jose Mourinho kutumia viatu
vya Scott McTominay kuficha pesa za Paul Pogba.

Ghafla anaonekana kutokuamini kuhusu nguvu ya pesa, hili ni jambo geni
sana kwa Jose Mourinho ambaye tangu tumfahamu kwenye tasnia hii ya
ukocha tumemfahamu kama kocha anayeamini pesa ina nguvu ya kuleta
ushindi na makombe ndani ya timu

Muda huu akaonekana Jose Mourinho asiyekuwa mvumilivu na pesa,
hakutaka kukaa na kuendelea kusubiri pesa zitakuja kumletea magoli na
pasi za mwisho alichokifanya ni kugeuka upande wa pili na kumchukua
Scott McTominay.

Akaweka imani kubwa juu yake, kitu kizuri alipoaminiwa kijana wa watu
hakuonesha kumwangusha kocha wake aliyemwamini, akawa anafanya kitu
kulingana na alichokuwa ameagizwa kufanywa na kocha.

Huu ndiyo msingi wa Jose Mourinho kila anapopita, hutaka kuona
mchezaji akifanya vitu vingi anavyomwagiza mchezaji ndani ya uwanja.

Alipokuwa anatakiwa kukaba alikuwa anakaba kweli na hii ndiyo furaha
ya Jose Mourinho kuwa na timu inayokaba sana.

Alipotakiwa kuipandisha timu alifanya kama alivyoelekezwa kwa kiwango
kikubwa na utulivu mkubwa ndani yake na hakutengeneza uwazi mkubwa
kati yake na Nemanja Matic katika eneo la katikati mwa uwanja.

Ukomavu mkubwa ukawa unaonekana ndani yake, akawa anafanya maamuzi ya
kikubwa tofauti na umri wake, alifikia hatua mpaka hatua ya kuilisha
familia yake bila kujali umri aliokuwa nao, kikubwa nidhamu
ilimuongoza.

Nidhamu ambayo ilimfanya atimize jukumu lake ipasavyo uwanjani. Ikawa
kawaida kumuona Paul Pogba akianzia benchi ndani ya michezo minne

Hata lawama za kwanini Paul Pogba haanzi zilipungua kwa sababu thamani
ya pesa ya Paul Pogba ilionekana ndani ya kiatu cha Scott McTominay.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

TUKITOKA BOTSWANA NA MISRI TUNATAKIWA KUFANYA YAFUATAYO

HOTUBA YA RAIS WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU ALIPOZUNGUMZA NA WAHARIRI WA HABARI ZA MICHEZO JUMATATU MACHI 19,2018 KWENYE HOTEL YA SEASCAPE.