in , , ,

UJIO MPYA WA KOCHA MAXIMO BONGO

Kuna habari za kurejea tena kwenye soka la Bongo kwa aliyekuwa kocha wa timu ya Taifa Mbrazil Marcio Maximo lakini safari hii sio kuinoa Taifa Stars, ni watoto wa Jangwani timu ya Dar es salaam Young Africans maarufa kama Yanga.

Maximo ni kocha ambaye atakumbukwa kwa mambo mengi kwenye soka la Bongo na machache kati ya hayo, ni namna alivyokuwa na msimamo kwa wachezaji waliokuwa na utovu wa nidhamu, kuhamasisha watanzania kuipenda timu yao ya taifa na kubwa kuliko yote, ni kuipeleka Taifa Stars kwenye michuano ya kombe la Afrika kwa wachezaji wa ndani maarufu kama CHAN.

Marcio Maximo
Marcio Maximo

Baada ya mkataba wa aliyekuwa kocha wa timu ya Yanga Hans Ven Der Pluijm kumalizika mwishoni mwa msimu uliomalizika hivi majuzi, kumekuwa na habari za wanajangwani hao, kumsaka mtu ambaye atakuja kuungana na kocha msaidizi wa timu hiyo Boniface Mkwasa ili kuirejesha timu hiyo kwenye makali yake baada ya msimu huu, kujikuta wakipoteza ubingwa wao mbele ya watoto wa mjini timu ya Azam dakika za lala salama.

Kama Mbrazil huyo atafikia makubaliano na kuja kuinoa timu hiyo, ni wazi kuwa atakuwa na faida kutokana na kuyafahamu vema mazingira na utamaduni wa watanzania. Maximo anajua kiwango cha wachezaji wa kibongo na umuhimu wa mechi kubwa kama “Kariakoo Derby” ambayo huwakutanisha timu za Simba na Yanga.

Kwa siku za hivi karibuni, Yanga ni mahali ambapo makocha wamekuwa hawakai muda mrefu kutokana pengine na sababu mbalimbali kama vile, maslahi na kutofikia malengo ya timu. Mashabiki wa timu hiyo kwa muda mfupi, wamemuona kocha Mbelgiji Thom Saintfiet na waholanzi Ernie Brands na Hans Van Der Pluijm ambaye amemaliza mkataba wake wa miezi sita.

Pamoja na kufanya mawasiliano na kocha Maximo, bado Yanga wanaendelea kusaka kocha mwingine ambaye atakuja kuwaletea mafanikio endapo makubaliano na Mbrazil huyo hayatofikiwa.Huu ni muda ambao mashabiki wa Jangwani wana hamu ya kujua mwalimu wao mpya kuelekea kuanza kwa ligi kuu ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu.

Report

Written by Oscar Oscar Jr

For about two years now, I have been writing and reporting different news regarding football to my own blog and to my facebook account and i have managed to attract a good number of audience.

My objective is to build career as a sport Pundit at a highly reputed and eminent media institution, to utilize my writing skills and experience to inform and entertain audience and to gain an opportunity of mastering the Art of writing and reporting sports news from more football Pundits.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Ulaya: Vita ya Real na Atletico Madrid

Real Madrid mabingwa mara 10