in , , ,

Uingereza kuzuia wasio na ujuzi kuingia

Priti Patel , waziri wa mambo ya ndani, mzaliwa wa Uganda

Uingereza inapanga kuwafungia mipaka wafanyakazi wasio na ujuzi na wale wasioweza kuzungumza Kiingereza, ikiwa ni sehemu ya mabadiliko makubwa ya sheria za uhamiaji, hatua itakayomaliza zama za wafanyakazi nafuu kwenye viwanda, maghala, hoteli na migahawa.

Serikali inasema kwamba inachukua hatua hii ya aina yake, fursa ya kipekee kwa ajili ya kudhibiti kabisa mipaka yake kwa mara ya kwanza na kuondosha dhana potofu iliyosababishwa na uhuru wa uhamiaji ndani ya Umoja wa Ulaya (EU).

Uingereza imeamua kujiondoa kwenye EU na sasa ipo kwenye kipindi cha mpito hadi mwishoni mwa mwaka huu, ikiweka mipango yake upya kwenye sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na soka, vigezo na masharti mapya kutolewa.

Hata hivyo, hatua hii inapingwa na viongozi wa viwanda lakini pia wapinzani wa kisiasa wakiwamo vyama vya Labour na Liberal Democrats, wakisema hatua hiyo ni mbaya na yenye athari hasi kwa uchumi, wakisema kwamba itarajiwe kufungwa kwa viwanda, maduka na watu kupoteza kazi.

Watu wa viwanda wanasema kwamba mabadiliko hayo yatakuwa na athari kubwa kwenye maeneo kama ya kuchakata vyakula viwandani, kazi inayotegemea kwa kiasi kikubwa wafanyakazi kutoka nchi za EU kuhakikisha rafu za maduka makubwa zinajaa chakula kwa ajili ya mahitaji makubwa ya wakazi wa nchi hii.

Unison – chama kinachowakilisha wafanyakazi wa sekta ya afya, kinasema kwamba hatua hiyo ni hatari na ni janga kabisa na kwamba itaacha hali mbaya kwenye eneo la utunzaji wagonjwa na wazee.

Hata hivyo, mawaziri wanasema kwamba wanatekeleza mpango wa kuondoka EU – Brexit kama ulivyoombwa na wapiga kura na kwamba ni wakati wa biashara kujipima na kuachana na wafanyakazi nafuu au rahisi.

Waraka wenye kurasa 10 unaainisha baadhi ya sera mpya za uhamiaji kuwa ni mipaka ya Uingereza kufungwa kwa wasio na ujuzi na kwamba wahamiaji wote lazima wazungumze Kiingereza; anayetaka kuingia na kuishi Uingereza lazima awe na ofa ya kazi na mshahara uwe walau pauni 25,000 kwa mwaka japokuwa atakayelipwa pauni 20,480 atafikiriwa katika mazingira maalumu kwa maeneo yenye upungufu wa watu na ustadi kama unesi.

Hapatakuwapo tena nafasi kwa watu kuja kujiajiri wenyewe hapa; wadhibiti mipakani hawatapokea tena vitambulisho kutoka nchi kama Ufaransa na Italia; ustadi wa wageni wanaotaka kufanya kazi Uingereza utashushwa kutoka ngazi ya shahada hadi A-level.

Hata hivyo, haki ya kuingia na kufanya kazi kwa wasanii, waburudishaji na wanamichezo pamoja na wanamuziki itaachwa pale pale. Serikali itaanzisha kampeni kubwa na maalumu kuwaandaa waajiri kwa ajili ya mabadiliko hayo Januari mwakani wakati raia wa EU wataanza kuchukuliwa kama wageni kutoka nchi nyingine bila upendeleo wowote.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Soka: Maslahi ya mabepari yanavyoiua

Tanzania Sports

Liverpool watapindua meza Madrid?