in , ,

Tuziache stori za waamuzi, Simba ni timu bora hapa Tanzania

Timu ya soka ya simba

Moja ya ratiba ambazo nilikuwa naziona ngumu kwa Simba ni yeye kwenda kucheza katika viwanja vya kanda ya Ziwa.

Hii ndiyo ratiba ngumu sana ambayo nilikuwa naitazama kwangu mimi. Ugumu wa ratiba hii haukuja tu kwa sababu anaenda kucheza ugenini.

Hapana! Ugumu wa mechi hizi ulikuja na sababu tatu ambazo mimi nilikuwa naziona ni nzito na ambazo zinaweza kuifanya Simba isifanye vizuri kwa asilimia kubwa.

Lakini kwa asilimia tisini (90%) Simba ilifanikiwa sana kupata matokeo ambayo ni chanya kwake na matokeo ambayo yamemsaidia yeye kujikita kwenye hizi mbio za ubingwa.

Ngoja nikuambie kitu kimoja rafiki yangu. Simba alikuwa anaenda kucheza ugenini. Kwenye viwanja ambavyo alikuwa anakaribishwa kama mgeni.

Hii ndiyo sababu ya kwanza ambayo ilikuwa inatia ugumu kwenye mechi za Simba katika ukanda wa kanda ya ziwa.

Siyo kwamba tu Simba ilikuwa inaenda kucheza ugenini, pia ilikuwa inaenda kucheza na timu ambazo mara nyingi huwa zinakamia sana zinapokutana na hizi timu mbili kubwa hapa nchini (Simba na Yanga).

Ulikumbuka Yanga ambavyo walivyopata wakati mgumu kwenye mechi ya mwisho waliyocheza na Alliance Schools kwenye uwanja wa CCM kirumba?

Iliwalazimu Yanga wasubiri mpaka hatua ya penati ili kuwapa nafasi ya wao kupata ticketi ya kwenda nusu fainali ya kombe la Azam.

Achana na hiyo, Simba alikuwa anaenda kukutana na timu ambazo kwa asilimia kubwa ziko kwenye mstari wa kugombania kutoshuƙa daraja.

Alliance Schools hana maisha yenye furaha kwenye msimamo wa ligi kuu. Kagera Sugar maisha yake yanahesabika tu.

Biashara United hatuna uhakika kama atabaki kwenye ligi kuu ya Tanzania bara. Hapa ndipo ugumu mwingine ambao alikuwa anaenda kukutana nao Simba.

Yani kwenda kucheza na timu ambazo kwa asilimia kubwa zilikuwa zinapigana ili kutokushuka daraja.

Timu ambazo zilikuwa zinahitaji alama tatu kama pumzi yao ya mwisho. Timu ambazo akili mwao zilikuwa zinawaza ushindi tu.

Hapa unajua kipi hutokea unapokutana na timu za aina hii katika nyakati kama hizi tena katika mazingira ya uwanja wa nyumbani ?

Simpo tu, kukamiwa. Timu itakukamia kweli kweli, itacheza kwa nguvu kuhakikisha kuwa inapata alama tatu ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kubaki ligi kuu.

Hiki kitu nilikiona kabla, moyoni nikasema kuwa Simba anaenda kukutana na mechi ngumu sana katika ukanda huu uliozungukwa na Ziwa Victoria.

Ukanda ambao upatikanaji wa Samaki huwa ni kwa wingi sana. Ukanda ambao Simba alitakiwa kucheza mechi moja kila baada ya siku mbili.

Hapa ndipo ugumu mwingine ambao ulikuwa unaonekana kwenye mechi za Simba. Hawakuwa na nafasi ya wao kupumzika.

Hawakuwa na nafasi ya kufikiria kwa upana na kwa muda mrefu kuhusiana na mechi ambayo ilikuwa inafuata kwao.

Yani muda ambao walikuwa nao ni kula, kulala , kusafiri na mechi. Muda ulikuwa finyu sana kwao. Muda ambao hata benchi la ufundi ni vigumu kupata muda sahihi wa kuisoma timu pinzani kwa mechi inayofuata.

Lakini ndivyo hivo, haikuwa na jinsi. Walitakiwa kabisa kucheza mechi moja kila ɓaada ya siku mbili. Hili halikuwa na mjadala kabisa.

Kazi kubwa ikabaki kwao kujibu swali moja tu. Watamalizaje hizi mechi wakiwa na matokeo chanya? Hili ndilo swali kubwa na zito lililokuwa linawasumbua Simba.

Lakini mwisho wa siku walilijibu vizuri sana. Simba imefanikiwa kupata alama tisa(9) kati ya alama kumi na mbili (12 ) katika ukanda wa Ziwa.

Wametumia njia gani ?. Ni wao kuhakikisha wanabadilisha kikosi mara kwa mara. Wakati ligi inaanza msemaji wao aliwahi kusema Simba ina kikosi kipana.

Inaweza kucheza mechi mbili ndani ya siku moja na ikapata matokeo ambayo ni chanya. Hiki alikisema lakini tukamuona ni mjivuni sana.

Maneno yake yamekuja kujidhihirisha katika mechi hizi ambazo wamecheza katika ukanda wa Ziwa.

Timu imefanikiwa kubadilisha kikosi vizuri ili kuendana na ratiba ngumu, ratiba ambayo ilikuwa inawahitaji wao kucheza mechi moja kila baada ya siku mbili.

Na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupata matokeo yenye faida kwao tena katika mazingir ambayo wengi waliona ni mazingira magumu kwa Simba.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Katikati ya furaha ndiko kulikuwa mwisho wa Alexis Sánchez

Tanzania Sports

Wakati tunamfurahia Kelvin John, tumsaidieni na Nkomola