in , , ,

TETESI ZA USAJILI LEO

 

Juventus kumnasa Sterling

 

Miamba wa Italia, Juventus, wapo tayari kutoa pauni milioni 50 kumnasa mshambuliaji wa Liverpool, Raheem Sterling.

 

Juventus wameingia kwenye vita ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anayesita kusaini mkataba mpya na Liverpool huku akitakiwa na klabu nyingine kadhaa.

 

Inaelezwa kwamba wakimnasa Sterling wanaweza kumwachia kiungo machachari, Paul Pogba kurejea Manchester United au kwenda au Chelsea.

 

Inaelezwa kwamba kiangazi hiki huenda wachezaji hadi 10 wakaondoka Liverpool, wakiwamo mabeki Glen Johnson, Martin Skrtel na Kolo Toure.

 

Wengine ni nahodha Steven Gerrard ambaye mkataba unaisha na anakwenda Marekani, Sterling ambaye huenda akauzwa. Wengine ni Javi Manquillo, Mario Balotelli, Fabio Borini na Rickie Lambert.

 

Mshambuliaji wa PSV Eindhoven ya Uholanzi, Memphis Depay, 21, huenda akajiunga na Liverpool, japokuwa anatakiwa pia na Manchester United.

 

Manchester City wanaelekea kumkosa kiungo wa Wolfsburg, Kevin de Bruyne anayesema kwamba anataka kubaki nchini Ujerumani.

 

Taarifa kutoka Hispania zinasema kwamba kipa wa Manchester United, David De Gea, 24, atajiunga na Real Madrid kiangazi hiki, akirudi katika mji aliozaliwa.

 

Kocha anayeondoka Borussia Dortmund, Jurgen Klopp amekataa ofay a kuchukua nafasi ya Sam Allardyce katika klabu ya West Ham.

Inaelezwa kwamba Allardyce aliyeshika nafasi hiyo tangu Juni 2011 huenda akahamia Marekani kufundisha soka.

 

 

Kiungo wa Newcastle, Jonas Gutierrez, 31, huenda akaondoka klabuni hapo baada ya kuripotiwa kutokea mzozo baina yake na Kocha John Carver. Raia huyo wa Argentina ametoka kupona saratani mauzi na mkataba wake unamalizika, ambapo kocha hataki kumpa mpya.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Ni Arsenal na Villa fainali

Bayern, Barcelona wapeta UCL