in

Tetesi za usajili Bongo ‘Deal done’

Usajili wa Yanga

Tupo katika kipindi cha dirisha la usajili Tanzania vilabu mbalimbali vimekuwa vikihaha kuhitaji saini za wachezaji wazuri kuweza kuziba mapengo yaliyoonekana katika msimu ulioisha.

Ikifika kipindi hiki habari kubwa zinawajumuisha Simba na Yanga japo hivi sasa Azam FC nayo imejipenyeza usajili wake unavutia kuusikiliza kutokana na ubavu wa pesa timu hiyo iliyonayo.

Leo hii tunaangalia  usajili uliokamilika na wachezaji waliotangazwa na tetesi za usajili kuwa mchezaji yupi anaelekea wapi.

Cha kuvutia zaidi Yanga ambao wanahasiria kupoteza ubingwa miaka mitatu iliyopita sasa wanahitaji kujenga timu na kuweka majembe yatakayo isaidia timu kuelekea katika msimu ujao.

Huku wakijinadi kuwa hakuna unyongee tena bali wapenzi wa timu hiyo wawe na furaha sasa.

Tanzania Sports
Mchezaji mpya Wa Azam, Ally Niyonzima akiwa na Mkurugenzi Wa timu hiyo Abdulkarim Amin

Yanga hadi muda huu wa saa nane mchana wamefanya sajili  tatu zilizotangazwa huku tukiambiwa kuna wachezaji lukuki washasajiliwa ili kuziba mapungufu huku wakisema wazi kuwa kuna baadhi ya nyota watasepa.

Yanga tayari wamesajili beki tatu kutoka Polisi Tanzania Yassin Mustapha wote ikiwa miaka miwili.

Zawadi Mauya huyu kutoka Kagera Sugar ndiye aliyefungua dirisha la usajili kiungo mkabaji naye ashakula vyake kwa wananchi ujio wake unaweza kutia shaka juu ya viungo wakabaji waliopo.

Usajili mkubwa kabisa hadi sasa ni wa beki Bakari Nondo Mwamnyeto aliyekadiriwa kusajiliwa kwa dau la milioni 230 ni usajili bora kabisa kuwahi kutokea katika maisha yake.

Ni usajili ghali zaidi kwa wachezaji wa ndani wa Tanzania sasa ataungana na Kelvin Yondan na Lamine Moro Jangwani.

Tayari washapewa kila kitu maana ya mkataba ni pesa bwana unataka kuuliza hela wametoa wapi si kwingine pale GSM.

Tetesi kwa Yanga

Eric Lutanga  beki tatu kutoka Rayo Sports ya Rwanda naye anasadikika yupo katika rada za Wananchi.

Wengine ni Jesse Were  kutoka Zesco United pamoja na David Calabar Owino raia wa Kenya.

Pia kuna wachezaji wanatajwa kama Tuisila Kisinda pamoja na Tunombe kutoka DR Congo pale AS Vita.

Kwa wabongo kuna habari ya Wazir Junior baada ya kufanya vizuri ndani ya Mbao FC ila aliferi Azam FC sasa Yanga wanahitaji huduma yake.

Wakati mabingwa watetezi Simba SC nao kama kawaida yao kila ikifika majira ya saa saba nchana wanakuwa na jambo lao bado hawajatangaza kumsaini mchezaji yoyote ila tetesi zinasema kuwa Walter Bwalya kutoka El Gouna ya Misri.

Pia kuna habari za mchezaji wa Lipuli FC Duchu  ila hawa wakimaliza fainali kazi itakuwepo.

Tanzania Sports
Baada ya Kusaini

Je ungependa kusikia Benard Morrison akuhamia Simba au ukipata habari hii utajisikiaje basi subiri.

Azam FC wao nao wana jambo lao msimu huu tayari wamesajili nyota wawili Awesu Awesu kutoka Kagera Sugar huku Ally Niyonzima naye akijiunga huko kwa mkataba wa maiaka 2.

Lakini kama haitoshi Mkurugenzi wa Azam FC Abdulkareem Amini ameweka ujumbe katika ukurasa wake wa instagram kuwa shughuli bado inaendelea hakuna mapunziko.

Akimaanisha kuwa watatangaza mchezaji mwingine haraka iwezekanavyo baada ya kumtangaza Ayoub Lyanga kutoka Coastal Union.

Hebu tosheka na hizi kwanza tutaendelea maana mwaka huu mambo ni moto sanakatika usajili Mnyama huko akimaliza Fainali ndio tutajua naye anakipi cha kujibu.

Labda nieleze kidogo juu ya swali la nani anasajili Yanga ripoti ya kocha yupi , Msola  ambaye ndio Mwenyekti wa timu hiyo aliteua watu wa ufundi mwezi October mwaka 2019 bado hajalivunja lakini pia usajili wa bongo tunaujua jamani kocha huwa hashilikishwi kwa asilimia mia moja.

Hii itaisha baada ya kuingia katika mabadiliko hebu tutulie tuone wanaleta nini msimu huu.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
AUDIENCES

Performers Need Live Audiences

Beno Kakolanya

Kwanini Azam FC wasimsajili Kakolanya ?