in , , , ,

TENGA KUFUNGUA KOZI YA BEACH SOCCER

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga atakuwa
mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa kozi ya mpira wa miguu wa ufukweni (beach
soccer) itakayoanza kesho (Julai 9 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

Kozi hiyo itafanyika kwa wiki nzima kwenye klabu ya Escape iliyoko karibu
na Safari Carnival, Mikocheni karibu na makao makuu ya Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT)- JKT Mlalakuwa. Uzinduzi utafanyika saa 3 kamili asubuhi.

Washiriki wa kozi hiyo itakayokuwa chini ya wakufunzi kutoka Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ni 60 ambapo 30 ni makocha wa mpira wa
miguu na 30 wengine ni waamuzi wa mpira wa miguu.

Wakufunzi hao wa FIFA ni Angelo Schirinzi kutoka Uswisi kwa upande wa
makocha wakati George Postmar kutoka Uholanzi ndiye atakayewanoa waamuzi.

*PROGRAMU YA MAZOEZI YA TAIFA STARS*

Taifa Stars chini ya Kocha Kim Poulsen inaendelea kujinoa jijini Dar es
Salaam tayari kuikabili Uganda (The Cranes) katika mechi ya kufuzu kwa
Fainali za Afrika kwa Wazhezaji wa Ligi za Nyumbani (CHAN) itakayochezwa
Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

* *

*Ratiba ya mazoezi kwa Taifa Stars ni kama ifuatavyo;*

Jumanne- Julai 9 mwaka huu Saa 9 alasiri Uwanja wa Taifa

Jumatano- Julai 10 mwaka huu Saa 9 alasiri Uwanja wa Taifa

Alhamisi- Julai 11 mwaka huu Mapumziko

Ijumaa- Julai 12 mwaka huu Saa 10 jioni Uwanja wa Taifa

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

THE FIRST EVER CAVB NATIONAL VOLLEYBALL REFEREEES COURSE ENDS IN DAR

*HAKUNA HILA KWENYE MAREKEBISHO YA KATIBA- TENGA*