in , , ,

Taifa Stars yaichapa Zimbabwe 1-0

TIMU ya soka ya Tanzania leo Jumapili imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zimbabwe katika mchezo wa kwanza w  kusaka tiketi ya kushiriki fainali zijazo za Kombe la Afrika uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Bao hilo pekee  lilipatikana kupitia kwa mshambuliaji, John Bocco, katika dakika ya 15 ya mchezo huo.

Mfungaji huyo anayechezea timu ya Azam alifunga baada ya kuunganisha krosi safi ya Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

 

Mechi hiyo ilikuwa na ushindani kwa pande zote mbili hasa Taifa Stars walioonekana kutoridhika na bao hilo moja na kufanya mashambulizi kadhaa katika lango la wapinzani wao.

Mbwan akiwa kazini
Mbwana akiwa kazini

 

Dakika ya 19 Taifa Stars ilifanya shambulizi lingine kupitia kwa Ulimwengu lakini Bocco alichelewa kuunganisha krosi iliyopigwa na nyota huyo aliyepatika kutoka timu ya vijana ya umri chini ya miaka 17 ya mkoa wa Dodoma .

Kipindi cha pili timu zote zilionekana kushambulia kwa kasi na kurekebisha makosa lakini makipa wa timu hizo walikuwa makini kudaka na kulinda nyavu zao.

 

Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij,amefurahishwa na ushindi huo na kuahidi kwamba bado wana kazi ya kujijenga.

Nooij alisema ushindi haukuwa rahisi kwa sababu wapinzani wao walitaka kupata bao au ushindi wa ugenini.

 

Naye kocha mkuu wa Zimbabwe, Ian Gorowa, alisema kikosi chake hakikuwa na bahati na licha ya kufungwa walicheza vizuri.

Gorowa alieleza kwamba watahakikisha wanashinda nyumbani kwao na kusonga mbele.

Kikosi cha Taifa Stars kilikuwa: Deogratius Munishi, Shomari Kapombe, Oscar  Joshua, Nadir Haroub ‘ Cannavaro’, Kelvin Yondani, Frank Domayo / Amri Kiemba (dk 71), Mrisho Ngassa / Haroun Chanongo ( 77), Mwinyi Kazimoto, John Bocco/ Khamis Mcha( dk 85), Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu.

Zimbabwe :George Chigova, Partson Jaure, Danny Phiri, Hardlife Zvirekwi, Stephen Alimenda, Tendai Ndoro, Milton Mkube, Kudakwashe Mahachi, Cuthbert Malajila, Peter Moyo na Eric Chipeta .

 

 

Mechi hiyo ilichezeshwa na mwamuzi , Joseph Odartei Lamptey kutoka Ghana.

Taifa Stars na Zimbabwe zitarudiana baada ya wiki mbili na mshindia ataivaa Msumbiji au Sudan Kusini .

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Arsenal FA Cup Winners Parade 2014

Atletico mabingwa Hispania