in , , ,

TAIFA STARS YAANZA KUJINOA ADDIS ABABA

Taifa Stars imetua jijini Addis Ababa, Ethiopia leo (Mei 28 mwaka huu)
alfajiri kwa ndege ya EgyptAir ambapo itaweka kambi ya wiki moja kujiandaa
kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco (Lions of the Atlas)
itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech.

Stars iliyotua na kikosi cha wachezaji 21 imefikia hoteli ya Hilton, na
imeanza mazoezi leo (Mei 28 mwaka huu) saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Addis.

Kwa mujibu wa Kocha Kim Poulsen, Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager itakuwa na vipindi (sessions) vinne vya mazoezi kabla ya
kucheza mechi ya kirafiki na Sudan (Nile Crocodile). Mechi dhidi yan Sudan
itachezwa Jumapili kuanzia saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Addis.

Sudan ambayo pia imeweka kambi yake Addis Ababa kujiandaa kwa mechi ya
mchujo ya Kombe la Dunia ilicheza mechi yake ya kwanza jana (Mei 27 mwaka
huu) dhidi ya wenyeji Ethiopia na kulala mabao 2-0.

Wachezaji wanaounda Stars ni nahodha Juma Kaseja, nahodha msaidizi Aggrey
Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto
Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis
Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent
Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi.

Kikosi hicho kinatarajiwa kuondoka Addis Ababa kwenda Marrakech alfajiri ya
Juni 3 mwaka huu kwa ndege ya EgyptAir. Stars itatua siku hiyo hiyo
Casabalanca na kuunganisha moja kwa moja kwenda Marrakech.

Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Crystal Palace watua Ligi Kuu

Request to the Government for construction of a 50-meter swimming pool