in , , ,

Kashfa riadha yashika kasi..

 

Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) imetaka hatua za kinidhamu kuanza kuchukuliwa mara moja dhidi ya wanariadha wa Urusi wanaodaiwa kutumia dawa za kusisimua misuli ili kuibuka washindi.

IOC imelitaka Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Riadha (IAAF) kuchukua hatua baada ya ripoti kutolewa kwamba ilikuwa kama mtindo kwa wanariadha wa Urusi kutumia dawa hizo, ikidaiwa pia kwamba viongozi au makocha wao wanajua vyema.

Hatua hiyo inakuja wakati kamati huru iliyoundwa na shirika linalopigana dhidi ya dawa hizo – Wada – kutaka Urusi ipigwe marufuku kwenye mashindano ya riadha, kutokana na kile kinachoonekana kwamba serikali ilikuwa ikiunga mkopo mpango wa kutumia dawa husika.

Baadhi ya waliotajwa kwenye ripoti hiyo kwa kujihusisha na kashfa ya kutumia dawa za kuongeza nguvu ni Mariya Savinova, aliyetwaa medali ya dhahabu kwenye mbio za mita 800 za Olimpiki jijini London 2012, sambamba na Ekaterina Poistogova, aliyetwaa shaba kwenye mbio hizo hizo.

Anastasiya Bazdyreva, Tatjana Myazina na Kristina Ugarova ni wanariadha ambao pia walitajwa, japokuwa tuhuma dhidi yao hazikuthibitishwa na hadi asubuhi ya leo watano hao walikuwa bado kuwasilisha majibu juu ya matokeo ya utafiti uliofanyika.

Advertisement
Advertisement

Wada inasema kwamba mashindano yale ya London 2012 yalihujumiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na waliotakiwa kuratibu uchunguzi na ubainifu wa wanaotumia dawa walifanya makusudi na kukaa kimya walipotakiwa kusema, na kuondoka walipotakiwa kukaa, hivyo washindi wasio halali wakapatikana.

Ikulu ya Urusi, maarufu kama Kremlin, imekana madai yote hayo na kusema yanayozungumzwa dhidi ya taifa hilo hayana msingi. Wapo wengine, hata hivyo, wanadai kwamba utumiaji wa dawa za kusisimua misuli si kwa Urusi pekee, hivyo hatua za kweli zingechukuliwa zingenasa wengi.

Hata hivyo, kwa sasa mzigo upo kwa Urusi ambao wamebainika kujihusisha na tabia hiyo iliyowanyima watu waadilifu kupata ushindi kwenye mbio. Hali hii inamwelekea moja kwa moja Rais wa IAAF, Lord Coe, Mwingereza.

Lord Coe anasema kwamba wamelielekeza Shirikisho la Soka la Urusi (Araf) kutoa maelezo yake juu ya madai hayo kabla au ifikapo mwishoni mwa wiki hii. Anasema kwamba baada ya kupitia mrejesho watakaopata ndipo IAAF itakapoamua hatua gani zichukuliwe, zinazoweza kufikia kufungiwa ushiriki kwenye michezo.

Taarifa ya IOC kuhusu suala hilo inasema: “Sera yetu ni kutovumilia matumizi ya dawa za kuongeza nguvu hata kidogo, hivyo baada ya kukamilika kwa mchakato huu, IOC itachukua hatua zinazotakiwa kuhusiana na kupokonya na kutoa upya medali kwa wanaohusika. Kutegemeeana na hali halisi,”

Rais wa IOC, Thomas Bach, amenukuliwa na kituo cha televisheni cha New Zealand akisema kwamba anatarajia Urusi watatoa ushirikiano katika mchakato unaoendelea, kupokea na kutekeleza maelekezo ya Wada ili kuhakikisha wanashiriki michuano ya Rio 2016.

Kadhalika, Bach aliongeza kwamba matarajio yake ni kwamba Lord Coe atafanya kila kitu kinachotakiwa kwa ajili ya kuusafisha mchezo huo. Kashfa hii kubwa inakuja wakati kwenye soka kukiwa na kashfa ya uozo mkubwa kwenye Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kuhusu rushwa, wizi na utakatishaji wa fedha kwa miongo kadhaa.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Platini aandaliwa njia

Tanzania Sports

Blatter alazwa hospitali