in , , ,

Soka: Mkataba wa kocha una thamani ya karatasi uliochapiwa

Katika sekta ambayo makocha hufutwa kazi mara kwa mara na kutupwa ghafla, na kwenye msimu ambao Watford wamewafukuza kazi makocha Javi Gracia na Quique Sanchez Flores ndani ya siku 86 tu kauli ya kwenye kichwa cha habari ni ya kutazama sana.

Kwa wanasheria kama Ray Wann, kazi yao ni kuhakikisha kwamba hali hii ndiyo inatokea kwa wateja wao. Wann amebobea katika mikataba ya kiutendaji akiwa na kundi la kisheria linaloitwa Sheridans.

Kazi yao ni kupambana na kuhakikisha haki za wateja wao, na kwa miaka kadhaa sasa, Wann amefanya kazi kwa wote – klabu na makocha kwenye kujadiliana juu ya mikataba kabla ya kusainiwa au mwishoni mwa michakato ya mikataba yenyewe – inapoelekea kuvunjwa.

Kimsingi, ni uvunjaji wa mikataba hii unaovuta na kupamba vichwa vya habari, hasa kutokana na kuvunjwa kwa ghafla na pia suala la kima cha malipo kama fidia ya kuvunjwa. Lakini kazi kubwa hufanywa mwanzoni.

Naam, hufanywa awali kabisa wakati yapo matumaini makubwa nay a hali ya juu na uhusiano baina ya klabu na kocha mpya wao mtarajiwa ukiwa mzuri na wa kusisimua.

“Kwa kiasi kikubwa, yote hufanyika kama kawaida,” Wann anaiambia tanzaniasports. “Kama ilivyo kwa mkataba wowote ule, kuna masharti ya kukubaliana baina ya mwajiriwa na mwajiri. Mfumo ni kana kwamba ni ule ule, japokuwa ni wazi panakuwapo tofauti hapa na pale,” anaongeza Wann.

Katika ajira rasmi inayokidhi viwango, haki za kisheria ndicho kitu cha chini kabisa unachokuwa na uhakika nacho chini ya sheria za Uingereza. Kwa maana nyingine ndiyo dhamana kwa ajili ya kulinda pande zote mbili.

Kati ya hizo za msingi kabisa ni tamko la kimaandishi juu ya ajira, likizo na vitu vingine vya aina hiyo. Lakini katika soka, haki hizo kwa kiasi kikubwa zinazidiwa na vifungu mbalimbali vinavyobuniwa wakati wa kutengeneza mkataba wowote.

“Haki za kisheria, baada ya kuzingatia yote na kwa kiasi kikubwa, zinahusika na mwajiriwa wako wa kawaida ambaye analipwa, tuseme, pauni 80,000 kwa mwaka. Makocha wa soka, hata hivyo, hutokea wakapata kima kikubwa sana juu ya hicho. Haki hizo, ambazo bado zina maana, ni ndogo sana ikilinganishwa na kile kilichoandikwa kwenye mkataba,” anasema Wann.

Mapema, klabu watakuwa wameshafanyia kazi kwamba ni kiwango gani cha fedha watakachotakiwa kumlipa kocha nje ya mkataba wake katika hatua mbalimbali za muhula wake; kwa kiasi kikubwa kinakuwa kinahusiana na mambo ya ufanisi katika utendaji kazi. Ni kwenye hali ya mwenendo mbaya wa utendaji kazi unaoweza kusababnisha fidia isilipwe.

“Watu wengi wana maoni kwamba klabu huwa zinafanya ukatili au kuwakosea haki makocha linapokuja suala la fidia. Lakini ni tofauti kabisa kwa hakika. Pia kuna maoni potofu kwamba mkataba ukimalizika ndani ya mwaka mmoja tu kati ya mitatu, kwa mfano, basi kocha anapokea malipo ya miaka miwili iliyobaki. Sivyo,” mwanasheria huyu anasema.

Sasa basi, ni kitu cha namna gani hutokea na hali huwa vipi kwa kocha kufukuzwa kazi? “Watakachokuwa wameweka, labda ni mfumo wa malipo ya kiangushio. Hayo yanalenga kushughulikia hali hiyo ikiwa muhula mzima wa mkataba hautamalizika. Husomwa kabla na makocha hupata kiwango fulani ya hicho. Mkataba unaomalizika miezi 18 kabla waweza kuishia kwa malipo ya miezi 12 au tisa tu na kiwango hushuka kutoka hapo,” anabainisha.

Kwa mfano, Jose Mourinho alipoondoka Manchester United miaka miwili na nusu kabla ya kumalizika kwa mkataba wake wa miaka mitatu, kiwango cha malipo kilichokuwa kimewekwa cha pauni milioni 15 kwa ajili yake na jopo la wakufunzi wake watano, kingepungua iwapo klabu wangesubiri hadi Februari 2019 badala ya walivyofanya kwa kutaka aondoke Desemba 18, 2018.

“Ukichukulia hali ya Jose, ni kwamba alitumikia muda mrefu wa mkataba wake. Katika hali hiyo, malipo ya kuvunjiwa mkataba yangekuwa kidogo zaidi. Na hapo ndipo fitina inaingia kwa sababu si lazima malipo husika yawe yanashabihiana na haiba husika. Inategemea tu kipi kilichokubaliwa awali,” anasema Wann.

Licha ya uwezekano wa kuwapo idadi mbalimbali au kubwa za fidia, huwa kuna malipo mengine ya dharura yanayokuwa yamekubaliwa wakati wa kuanza mchakato. Hayo ni pamojana ada kwa ajili ya kuhama eneo moja kwenda jingine, kuhakikisha familia ya kocha inahudumiwa kuendana na hali ya maisha na shule pamoja na kingine chochote kinachoweza kusaidia kuufanya mkataba wenye kupendeza.

“Kumbuka, klabu huwa ndizo zinahitaji makocha ili wawaajiri na kuwa nao, bila kujali hatua zinazoweza kuchukuliwa. Viwango hivyo vya fedha huwasaidia kuhakikisha kwamba wanawezeshwa kupita kipindi cha mpito kwa urahisi kadiri inavyowezekana. Ni mchakato,” anasema.

Hatimaye, kipengele chochote kilichokubaliwa kabla ya kocha kutia saini mkataba lazima kihakikisha kwamba, ikitokea hali mbaya, basi mapumziko yanakuwa rahisi kadiri inavyowezekana bila kujali kilichosababisha mtifuano baina yao. Mara nyingi, anasema Wann, mwanasheria aliyeshiriki kwenye mjadala wa awali huitwa tena mezani wakati mkataba unapoelekea kuvunjwa.

“Kila kitu kinakuwa kimetazamwa na kuamuliwa mapema, na kwa hakika, inakuwa kana kwamba kuweka alama ya vyema kwenye vile viwango vya nyongeza. Matarajio ni kwamba kwa ajili yako na ya kocha ni kwamba uwe umeshafanya kazi yako na kuweka mambo sawa tangu mwanzo!” anamalizia.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Arsenal wanaweza kurudi Ligi ya Mabingwa Ulaya

Tanzania Sports

Soka imeharibiwa isivyo kifani