in

Simba wanatangaza ‘utamu’ wa Ligi Kuu Tanzania

SIMBA SC

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wamecheza mechi ya tatu ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika dhidi ya El Merreikh ya Sudan wikiendi iliyopita. Katika mecho huo Simba waliwalazimisha wenyeji wao El Merreikh na kutoka nao suluhu.

Kwa matokeo hayo Simba wamefikisha pointi 7 katika kundi lao la A huku wakifuatiwa na mabingwa watetezi, Al Ahly ambao katika mechi mbili walizocheza wamevuna pointi 3 dhidi ya El Merreikh. 

Simba wao walianza kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS Vita, kabla ya kuwatandika mabingwa watetezi Al Ahly  1-0. Kisha kutoka 0-0 dhidi ya El Merreikh. 

Wakati naandika makala haya Al Ahly walitarajiwa kumenyana na AS Vita katika mchezo wa tatu wa mfululizo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa matokeo ya Simba wanahitaji ushindi wa mechi moja tu nyumbani dhidi ya AS Vita ya DR Congo au El Merreikh ya Sudan kuweza kufuzu hatua ya robo fainali. Mechi za AS Vita na El Merreikh bila shaka hazikuwa nyepesi lakini Simba wanajivunia ushindi wao dhidi ya Al Ahly na kuzitangazia timu zote zinaokwedna kucheza uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam zisitarajie kupata ushindi wowote.

NINI MAANA YA USHIRIKI WA SIMBA?

Tanzania Sports
Wakati mzuri kwa Simba Uwanjani

Katika kandanda Afrika mashariki kwa nyakati tofauti timu zimekuwa zikibuka na kupotea. Simba imekwua na rekodi nzuri ya mashindano ya kimataifa, lakini msimu huu wanaonekana kujivunia uzoefu waliopata kwenye mashindano hayo.

Mwaka 1998 Yanga wakiwa na kocha Tito Mwaluvanda na Raul Shungu walifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali Klabu Bingwa Afrika kwa mara ya kwanza.

Simba wanaweza kuweka rekodi ya kuwa timu pekee ya Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki kuweza kuingia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, tangu mfumo wa mashindano hayo ulipobadilika mwaka 2017 ambapo kuliwekwa hatua moja ya mtoano badala ya ile ya makundi kumalizika ikawa ya robo fainali, ikifuatiwa na nusu fainali na kisha fainali.

Hadi sasa mafanikio ya Simba ni jambo la kujivunia kwa Watanzania na Afrika Mashariki. Ikumbukwe Simba ndiyo klabu ya kwanza Tanzania kutoa mchezaji ambaye alikuwa miongoni mwa wafungaji bora wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2019. Emmanuel Okwi alikuwa alikuwa mchezaji aliyewakilisha Simba wakati huo na Ligi Kuu Tanzania bara. Hatua ya mchezaji kutoka Afrika mashariki kuwa miongoni mwa wafungaji bora ulikuwa ujumbe juu ya kuinuka kwa soka Afrika mashariki.

Ukanda wa Afrika Mashariki haujawahi kuwa na rekodi kubwa za kandanda kama kanda za Afrika magharibi,kusini na kaskazini. Lakini sasa Simba wamebeba matumaini makubwa ya washabiki wa ukanda huo.

Klabu nyingi za Afrika mashariki hazina nguvu kama zile za Al Ahly, Esperance, CR Belouzdad, Wydad Casablanca, Kaizer Chiefs, Mamelodi Sundowns, Raja Casablanca, Zamaleko,Ismailia,Orlando Pirates, Club Africain na nyinginezo.

Gor Mahia wamewahi kutinga hatua ya robo fainali katika Kombe la Shirikisho mara mbili 2017/2028 na 2018/2019). Yanga  walitinga hatua ya robo fainali mara moja sawa na Rayon Sports ya Rwanda (2018) lakini pia KCCA ya Uganda imefanya hivyo mara moja (2018)

Pesa za Ligi ya Tanzania

Tanzania Sports
Heka heka uwanjani

Wachezaji wa kigeni wamezidi kumiminika katika Ligi Kuu Tanzania.  katika kikosi cha Simba kilichoanza dhidi ya El Merreikh kilikuwa na wageni Francis Kahata (Kenya), Joash Onyango (Kenya) Taddeo Lwanga (Uganda), Chris Mugalu (DR Congo), Clatous Chama (Zambia), Larry Bwalya (Zambia), Luis Miquissone (Msumbiji) Lokosa (Nigeria) na Pascal Wawa (Ivory Coast) ni miongoni mwa nyota wanaowika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Wachezaji wengine wa kigeni waliko katika klabu ya Yanga ni Carlos Calinhos (Angola), Michael Sarpong(Ghana), Lamine Moro (Ivory Coast), Farouk Shikalo (Kenya), Yacouba (Togo).

Mwingine ni mshambuliaji nyota wa Namungo FC Stephen Sey raia wa Ghana ambaye amekuwa maarufu Ligi Kuu Tanzania Bara na kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika ambako mabao yake yameiwezesha Namungo kutinga hatua ya makundi.

Nyota hao watachagiza ongezeko la idadi kubwa ya wachezaji wa kigeni kutoka mataifa mbalimbali ambao bila shaka watakuwa chachu ya kuimarisha viwango vya wachezaji wazawa.

Aidha, nyota wa kigeni licha ya kusisimua Ligi Kuu Tanzania watavutia idadi kubwa ya wadhamini ambao watawekeza fedha zitakazosaidia klabu kujiendesha na kuboresha viwango vya wachezaji.

Mashindano ya CAF yanasaidia kuwaweka sokoni wachezaji wa klabu mbalimbali zinazoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara jambo linaloweza kuwa na faida kubwa kwao kuimarisha vipato vyao lakini pia kuongeza pato la nchi na hata klabu ambazo zinaweza kuongeza makusanyo yao kutokana na mauzo ya wachezaji husika kwenda katika klabu nyingine za nje ama ndani ya bara la Afrika.

Kwa sasa Ligi Kuu Tanzania kwa sasa ndio inaongoza kwa klabu kulipa mishahara mikubwa kwa wachezaji jambo ambalo limekuwa likivutia nyota wengi kukimbilia klabu mbalimbali zinazoshiriki Ligi hii.

Ushiriki wa Simba maana yake unatangaza mazuri ya Ligi ya Tanzania. vilevile wachezaji wake wengi ambao wanaitwa timu za taifa hivyo itawavutia makocha wengi kutaka kujua maendeleo ya wachezaji wao.

Report

Written by Mark Mpangala

*Markus Mpangala ni Mhariri, Mwandishi wa Makala Maalumu, Mwanahabari,Mwanablogu,Mwanafasihi na Mwanasafu, ambapo kwa kipindi cha miaka 12 amefanya kazi katika vyombo vya habari mbalimbali vikubwa na vidogo nchini Tanzania katika Michezo, Siasa, Elimu na utalii. Pia ni mchambuzi mchangiaji wa masuala ya siasa na utawala bora katika idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC SWAHILI). Ni mhariri na mhamasishaji wa usomaji wa vitabu*

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Yanga

FAIDA NA HASARA KAMA TIMU YA YANGA IKISHUSHWA DARAJA

cedric kaze

Mzuka wa ‘Kazelona’ wa Yanga ulivyozimwa