in

Simba Kuzitimulia Vumbi Yanga na Azam

mchezo wa soka, mahasimu wakiwa uwanjani

Sare ya Yanga dhidi ya Azam FC imetoa mwanya mkubwa kwa timu ya Simba kunyakua ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara zikiwa zimesalia mechi chache.

Kabla hatujapiga mahesabu ya ubingwa wa Simba, iko wazi kuwa Yanga na Azam zilitoa sare ya bila kufungana mchezo huo ulifanyika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Ikishuhudiwa magoli ya Azam FC yakikataliwa kwa kigezo cha mipira ya kuotea yaani ‘offside’, waamuzi wasaidizi bado watakuwa na la kuwaambia wapenda soka tatizo liko wapi katika kuona mipira ya kuotea.

Muamuzi wa kati Heri Sassii aliwanyima Yanga penati moja na Azam penati moja hivyo waamuzi ndio walioharibu mchezo ule.

Never Tigere na Mudathiri Yahya (Azam FC), Haruna Niyonzima na Bernard Morrison (Yanga) hawa wamecheza vizuri sana kila mmoja ameonesha nini amejaliwa.

Shabani Iddi (Azam FC) na David Molinga (Yanga) walionesha mchezo mbovu kabisa huku Chilunda akionekana kukosa utulivu anapofika kwa mwali pale golini.

Kocha wa Yanga Luc Aymael na Aristica Cioaba wa Azam wameleta radha ya vile viingilio kwa mashabiki mbinu zao zilikuwa na maana kubwa sana hadi kuona soka la aina ile.

Kituko katika mchezo huo mshambuliaji wa Yanga Yikpe Gislain amezomewa sana na shabiki wa Yanga , tumkumbushe tu kuwa Gareth Bale wa Real Madrid aliwahi kuzomewa ila amejibu kwa vitendo uwanjani huku Rafael Benitez hakuwahi kupendwa na shabiki wa Chelsea ila baada ya kuhudumu hapo aliwapa kombe la ‘Europa’ akawa katika midomo yao kwa nyimbo nzuri.

Bila kusahau Simon Msuva ambaye sasa anacheza Difaa El Jadida ya Morocco aliwahi kuzomewa sana juu ya uchezaji wake hii leo amebaki kuwa winga bora kwa miaka ya hivi karibuni.

Unamkumbuka Obrey Chirwa kwa sasa anacheza Azam FC ? Naye aliwahi kusemwa sana kutokana na dau lake kuwa kubwa na uwezo wake haukuwa mzuri mwanzoni baadae amekuwa kuwa mfalme.

Swali la kujiuliza kweli Yikpe anaweza kuwapa raha Yanga hadi wamuimbe, je mguuni Mpira anao au bado ni galasa kama wanavyosema Yanga wenyewe. 

Ni swala la muda tu, kama watampa nafasi aendelee kuhudumu au watamtolea nje asepe hilo lipo kwa uongozi wa Yanga.

Mpira ulikuwa mzuri wa aina yake kila timu ilijiandaa kimbinu pamoja  na saikolojia ya wachezaji wenyewe hii iliwafanya kujiamini na kuonesha kile walichotuandalia. 

Haya turudi nyuma sasa tuangalie ramani ya Simba kuelekea ubingwa wa ligi kuu Bara kwa misimu mitatu mfululizo endelea hapo chini.

Azam FC ambayo iko nafasi ya pili endapo ikishinda michezo yote minane iliyobaki utafikisha alama 82 huku Simba ikihitaji alama nane itangazwe kuwa bingwa.

Yaani  Azam ikishinda michezo yote minane itakuwa na alama 82 huku Yanga ikishinda yote itafikisha alama 80 wakati huo Simba ikishinda michezo mitatu inakuwa na alama 84 na kuwa bingwa bila kipingamizi.

Ila kwa sasa inahitaji alama 8 tu iweze kutangazwa kama bingwa kwa mara ya tatu mfululizo. Je ule usemi wa Haji Manara wa Simba kuwa watachukua mara kumi mfululizo ubingwa wa ligi una ukweli ndani yake ? au aulizwe baadaa ya msimu ujao.

Wengi watakuwa wanakosa ile misemo ya Haji Manara kuwaudhi Yanga , endapo watachukua ubingwa mapema zaidi basi tutashuhudia maneno mazito kutoka upande huo.

Report

Written by Amini Nyaungo

For the past 9 years, I have been working as the Sports news Journalist in online and print media this experience help me to be utilized by the different sports events where I have got chances to the media as the football pundit in different media in Tanzania.

What do you think?

74 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Tanzania Sports

Simba SC Kuukaribia Ubingwa

Dar young africans

Wazomeeni viongozi wa YANGA SIO YIKPE..