*Yakatwa mkia na Coastal Union
*Azam waendelea kuongoza ligi
*Spurs wapigana kuwapiga Saints

Wekundu wa Msimbazi, Simba Sports Club wamewakatisha tamaa washabiki wao baada ya kukubali kichapo cha 1-0 kutoka kwa Coastal Union ya Tanga.

Simba ambao walitarajiwa kupata pointi muhimu tatu kwenye mechi hiyo ya marudiano, walipwaya mno, hasa katika kipindi cha kwanza.

Licha ya Coastal kuwakosa wachezaji wake nyota karibu watano, chipukizi waliokuwa dimbani walitupiana mpira kama wenye uzoefu wa muda mrefu na kuwaadhiri Simba.

Bao la Coastal lilipatikana mwishoni mwa kipindi cha kwanza, ikiwa ni muda mfupi baada ya mwamuzi kumwamuru kipa Ivo Mapunda wa Simba kusogeza taulo lake alilokuwa ameweka golini na kutoa hisia tofauti juu ya uimara wake langoni.

Bao la Coastal lilifungwa na mmoja wa walinzi wake, Hamad Juma kutokana na pasi ya Razak Khalfan.

Kwa matokeo hayo, Simba wamejiweka katika nafasi ngumu ya kufuzu kwa nafasi mbili za juu kwenye ligi, kwa sababu kuna timu za Azama, Yanga na Mbeya City wanaofanya vyema.
Simba wapo nafasi ya nne baada ya kufikisha pointi 36 kutokana na michezo 22.

AZAM WAENDELEA KUTESA KILELENI

Katika mechi nyingine, Azam walipata ushindi mwembamba dhidi ya Oljoro JKT wa bao 1-0 lakini kwa umuhimu wake walichupa hadi pointi 47 kwenye msimamo wa ligi.

Bao la Azam lilifungwa na John Bocco katika kipute kilichofanyika nyumbani kwao Chamazi
Yanga wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 43 lakini lakini wana mchezo mmoja mkononi. Mbeya City wenye pointi 42 wanashika nafasi ya tatu.

SPURS WAPIGANA, WASHINDA EPL

20131108-054010.jpg

Katika mechi ya Ligi Kuu England (EPL), Tottenham Hotspur waliteseka lakini hatimaye wakaibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Southampton.

Kwa ushindi huo wa Spurs dhidi ya Saint, jamaa hao wa London Kaskazini wamefikisha pointi  56. Na wanashika nafasi ya 5, kwenye msimamo wa EPL.

Hata hivyo, kocha wao, Tim Sherwood ameshasema inahitajika kazi ya ziada kuweza kupata nafasi nne za juu ili kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL) badala ya Ligi ya Europa waliyoizoea na ambamo wameondolewa wiki iliyopita na Benfica wa Ureno.

Bao la dakika za mwisho la Gylfi Sigurdsson liliwapa ushindi huo Spurs.
Saints walitawala kipindi cha kwanza, wakipata bao kupitia kwa Jay Rodriguez kutokana na makosa ya Kyle Naughton.

Adam Lallana aliwapachikia Saints bao la pili kabla ya Christian Eriksen wa Spurs kupiga mabao mawili kusawazisha mambo, akiweka bao moja kila kipindi.

Ushindi huo umempa ahueni kocha Tim Sherwood ambaye ameshaanza kusemwa atafukuzwa na nafasi yake ikidaiwa itachukuliwa na Mdachi Louis van Gaal.

Hii ni mara ya kwanza tangu 2010 kwa Spurs kufanikiwa kutoka kufungwa mabao mawili na kuyarudisha na kupata ushindi, na ilikuwa dhidi ya mahasimu wao wa kaskazini mwa London, Arsenal, ambapo Spurs walishinda 3-2 kwenye ligi kuu.

Sasa Spurs wanashika nafasi ya tano wakiwa na pointi 56 wakati Everton walio juu yao, Arsenal wana pointi 62.

Manchester City wana pointi 63 na Liverpool 65 wakati vinara wa ligi, Chelsea wanazo 69.
Katika mechi nyingine, Stoke wamewaadhibu Aston Villa wasiotabirika kwa kuwafunga mabao 4-1.

Mkiani wamebaki Sunderland wenye pointi 25 sawa na Cardiff wakati Fulham wapo nafasi ya 20 kwa pointi zao 24.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Yanga wawapumulia Azam

Ronaldo: Marefa wanatunyonga