in , ,

Simba hawakujifunza kwenye mechi ya SOURA na Al Ahly

Moja ya timu bora barani Afrika ni Al Ahly, ni timu ambayo imedumu kwa muda mrefu ikifanya vizuri kwenye michuano mingi barani Afrika.

Wana fainali wa ligi ya mabingwa barani Afrika msimu jana. Moja ya watu ambao wamefanya mpira ni kazi. Kwao wao mpira ni zaidi ya Afya.

Ndiyo maana huwezi kushangaa kusikia kuwa wamesajili mchezaji kwa dau la bilioni 9, bajeti ya timu zote za ligi kuu Tanzania bara.

Kwao wao bajeti hii ya timu zote za Tanzania bara hupeleka kwa ajili ya kumsajili mchezaji mmoja tu. Hapo ndipo unapoona tofauti kati yetu na wao.

Kwetu sisi mpira ni kwa ajili ya kuimarisha Afya , wakati wao mpira ni kazi kama kazi zingine ambazo sisi huziona zina thamani kubwa.

Wao huwekeza kwa nguvu kubwa sana kwenye mpira, wakiamini kabisa watarudisha pesa zao na watapata faida kubwa.

Ndiyo maana wamekuwa wakifanya vizuri sana kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Na ndiyo timu ambayo huangaziwa kwa ukaribu kila michuano hii inapoanza na hupewa nafasi kubwa ya kubeba.

Ndiyo timu ambayo timu nyingi huombea kutopangwa nayo kwa sababu tu jamaa huwa wana biashara maalumu na michuano hii.

Wanajua namna ambavyo wanaweza wakapata matokeo bora kwenye michuano hii. Wanajua jinsi ya kucheza ugenini na nyumbani

Uliwatazama walipocheza dhidi ya Saoura? Kwenye uwanja wa ugenini?, waliwaheshimu sana wapinzani wao kwa sababu tu walikuwa nyumbani.

Hawakuwaheshimu kisa walikuwa bora zaidi yao, ila waliwaheshimu kwa sababu walikuwa nyumbani. Nyumbani ambapo wenyeji huwa wana faida kubwa kuzidi wageni.

Nyumbani ambapo mwenyeji ana mchezaji wa ziada ambaye ni shabiki. Ndiyo maana Al Alhly waliwaheshimu wapinzani wao.

Waliamini na wao wanaweza wakapata goli muda wowote, na ndicho kilichotokea. Al Alhly walikuwa nyuma kwenye mchezo huu mpaka pale walipowasazisha.

Al Ahly unaweza ukawaoana kama walicheza kawaida sana kwenye mchezo huu, lakini siyo kweli , walikuwa wametoa heshima kubwa kwa mwenyeji.

Na hii ndiyo siri kubwa sana kwa michuano hii. Ndiyo maana Al Alhly pamoja na umwamba wake bado wanaitumia.

Bado wakiwa kwenye viwanja vya ugenini hawafunguki sana ukilinganisha na kwenye uwanja wa nyumbani ambapo ndiyo sehemu ambayo hujidai.

Wao huwezi kuwaona wanajidai saaaana katika viwanja vya ugenini. Hiki kitu ndicho ambacho Simba walianza kukikosea katika mechi ya jana.

Wao hawakuwa na heshima kabisa na As Vita. Walijiona kama wapo katika uwanja wa Taifa. Walijiona kama wanaweza kucheza kama wanavyochezaga katika uwanja wa Taifa.

Hawakujua kutofautisha kucheza nyumbani na kucheza ugenini kabisa. Ndiyo maana walifunguka bila adabu.

Na As Vita wakatumia fursa ya wao kutoheshimiwa na Simba kufunguka kwa kuwafunga goli tano.

Simba bado ana michezo mingine miwili iliyobaki ambayo atacheza katika viwanja vya ugenini. Wanatakiwa kujifunza kwa Al Alhly.

Wanatakiwa kuwa na heshima kubwa sana wanapocheza katika viwanja vya ugenini. Wasijione wako katika uwanja wa Taifa kila Mara.

Madhara ya kutompa heshima mpinzani wako katika uwanja wake wa nyumbani ni yeye kukuadhibu bila huruma kama ambavyo As Vita walivyofanya.

Simba ni timu nzuri, na bado wana nafasi ya kufanya vizuri katika michuano hii, lakini wanachotakiwa kufahamu ni namna ya kucheza nyumbani na kucheza ugenini kwenye michuano hii.

Hapa ndipo ilipo siri kubwa ya mafanikio kwa timu nyingi. Timu nyingi huwekeza nguvu nyingi sana katika uwanja wao wa nyumbani.

Wakiamini kwenye uwanja wao wa nyumbani ndiyo sehemu ambayo wana nguvu kubwa kuanzia ya mashabiki kuliko kwenye viwanja vya ugenini.

Viwanja vya ugenini huwekeza nguvu kiasi kwa kumpa heshima mpinzani kitu ambacho husaidia timu kucheza kwa tahadhari na kwa uhakika mkubwa.

Na mwisho wa siku timu inaweza kujikuta imepata hata alama moja ugenini. Alama ambayo ni hazina kubwa sana kwenye michuano hii.

Alama ambayo hutumika kujumuishwa na alama ambazo timu hupata katika uwanja wa nyumbani.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Tumkabidhi rasmi Rashford jezi namba 10

Tanzania Sports

Unai anamuhitaji Ozil au Ramsey?