in

Siku Michael Edward aking’oka Liverpool

Michael Edward

Kila timu inapokuwa na mafanikio katika mchezo wa soka, kuna watu wanakuwa nyuma yake. Watu hao wanakuwa kama injini kwenye gari ambayo huwezesha shughuli nzima ya gari. 

Kwenye timu ni watu ambao wanahakikisha wachezaji wanakuwa katika mazingira mazuri ya utendaji wa kazi. Wanahakikisha makocha wanapata vifaa muhimu vya utendaji wa kazi. Wanahakikisha mfumo wa timu unalindwa na kuendelezwa kila siku. 

Si wao peke, bali wanao wasaidizi wao ambao wanajikita kwenye idara tofauti na kuwezesha shughuli za timu kwenda mbele zaidi. kwa Liverpool mtu huyo ni Michael Edward. 

Huyo ni mkurugenzi mtendaji wa Liverpool ambaye amepita nyakati nzuri na mbaya, lakini amesimama imara na kuifanya Liverpool kuwa timu inayojua kusimamia misingi yake. 

Kwa Michael Edward suala la weledi ndilo muhimu na ambalo limemfikisha kwenye kilele cha mafanikio. Liverpool ina mastaa wa kutajika. Liverpool inalipa mishahara mizuri. 

Liverpool wamepata mikataba minono. Loverpool wana kocha wa kiwnago cha juu cha dunia, Jurgen Klopp. Liverpool wanazalisha wachezaji kutoka kwenye akademi yao na msimu huu 2021/2022 wamekuja na kinda Elliot Harvey ambaye anaonekana wazi kuja kuchukua mikoba ya Mohammed Salah. 

Liverpool wametwaa mataji mbalimbali EPL,Ligi ya Mabingwa, Klabu bngwa dunia na Super cup. Liverpool imekuwa timu kabambe na mshindani mkubwa katika kuwania mataji EPL. 

Barani Ulaya Liverpoool bado inayo heshima yake ambayo imejijengea na inazidi kupanda ngazi kila kukicha. Liverpool wana mseto wa mastaa na wachezaji wa kawaida. 

Unaweza kuingiza fedha kwao kwa kununua vipaji kama Naby Keita, Sadio Mane, Mohammed Salah, Bob Firmino, Fabinho, Alexander Arnold, Allison, na wengine wengi ambao wanaweza kupata mafanikio kwenye klabu zingine. 

Hata baadhi ya watendaji wa Liverpool walipoondoka wengi walidhani huenda ikatetereka, lakini Jurgen Klopp na kikosi chake wameifanya Liverpool kuwa timu tishio na yenye kiu ya kushinda kila taji wanalowania. 

Msimu huu wanafukuzia mataji ya EPL,FA,Carabao na UEFA. Liverpool wapo kileleni mwa Ligi baada ya kucheza mechi 8 na kujikusanyia pointi 18 kutokana na ushindi wa mechi 5, sare 3 na hawajafungwa mchezo wowote msimu huu. 

Mbio za Liverpool kuwania taji zimekuwa za kila msimu na miaka mitano mfululizo wamekuwa wabishi wa EPL. Liverpool wametoa changamoto kwa timu zingine 17 na wanafukuzia ubingwa wa 20 ili kuwafikia rekodi ya watani wao wa jadi Manchester United. 

Sipati picha siku Liverpool wakifikisha idadi ya mataji 20ya EPL. Sipati picha Alex Ferguson atajisikiaje kushuhudia hilo angali hai kwani ni kitu ambacho amekuwa kikizuia kwa kuhakikisha anawafunga alipokuwa kocha na baada ya kuondoka kwenye ukocha anatamani Liverpoolwasifikie rekodi za Man United. 

Sasa, ushindi, mafanikio na ushindani wa Liverpool unasimamiwa na Mkurugenzi mtedaji Michael Edward. Iko hivi, Michael Edward mkataba wake unaelekea ukingoni, ambapo unatarajiwa kumalizika msimu huu. 

Nimesoma mahali mtandaoni ikielezwa kuwa Michael Edward haoneshi dalili za kutaka kuendelea kuwa kiongozi wa Liverpool. Zipo tetesi kuwa Michael Edward anaweza kuhamia nchini Hispania na kuongoza kigogo cha soka cha huko. 

Timu inayotajwa zaidi ni ile inayoongozwa na Florentino Perez yaani Real Madrid. Kwamba Perez anadaiwa kuvutiwa na utendaji na mafanikio ya Michael Edward na hivyo huenda akamvuta hadi Santiago Bernabeu kuwa bosi wa timu hiyo. 

Haifahamiki nafasi ya mkurugenzi wa sasa wa Real Madrid, Jose Angel Sanchez atakuwa wapi au ataondoka kumpisha Edward, lakini tetesi hizi si za kupuuzwa. 

Inaonekana licha ya Angel Sanchez kupata mafanikio ya kutwaa mataji ya La Liga na Ulaya ni kama kuna jambo limeyumba Real Madrid. Na kwmaba Michael Edward anaweza kwa suluhisho la uendeshaji wa timu hiyo. 

Kwanza Real Madrid ni kubwa kuliko Liverpool, lakini kuhimili na kuwabakiza mastaa kama Saio Mane,Salah,Virjil,Allison na kocha wao Klopp ni ishara ya uimara wa Michael Edward na kwamba hesabu zake zimeleta faida kubwa klabuni. 

Hilo la faida kubwa ndilo linalotafutwa na Florentino Perez. Vyovyote iwavyo ikiwa Michael Edward atatua Real Madrid kuwa bosi mpya maana yake kuna watu wataondolewa kwenye utendaji ili kuruhusu mwelekeo mwingine wa bosi. Hata hivyo suala la kuwalinda wachezaji wake Real Madrid sio jambo la kushangaza labda waamue kumuuza.

Pili, tetesi za usajili wa Kylina Mbappe nazo ni miongoni mwa mambo yanayoibua mjadala. Kwamba Liverpool ni miongoni mwa timu zinazotajwa tajwa kutaka kumsajili nyota huyo. 

Na kwamba kinara wa kusimamia dili hilo ni Michael Edward. Kwahiyo ili kuimarisha mipango ya Mbappe kusajiliwa Real Madrid maana yake inabidi achomolewe Michael Edward ili apelike mawazo yake Santiago Bernabeu badala ya kuyafanyia kazi Liverpool. 

Tatu, ikiwa hesabu hizo zitatimia na ndizo za kweli ina maana ushawishi wa Jose Angel Sanchez na Juni Calafat utakuwa umepungua kwa kiasi kikubwa kwani lazima bosi mpya atakuwa na mipango mipya yenye faida zaidi kwa klabu yake mpya. Na ndio mwanzo mpya.

Sijui itakuwaje siku Michael Edward aking’oka Liverpool, watabaki kileleni? Watampata mbadala wake makini? Hayo na mengine nayo yanatafakarisha.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Yanga FC

Yanga wanapanda na kushuka

Jwaneng Galaxy

Dakika 90 ‘Kwa Mkapa’ zilizowamaliza Simba