in ,

RVP aanza vibaya Manchester United

*Mashetani wekundu wapelekwa puta na Everton
 Na: Israel Saria
Tangu siku Sergio Aguero alipoifunga goli lililowapa Manchester City ubingwa wa England, washabiki wa Manchester United walisubiri kwa hamu msimu mpya.
Hawakuzipenda sherehe zile za ubingwa kwa tambo za majirani zao hao, na waliapa kwamba wangeanza kwa nguvu isiyo ya kawaida.
Kwa hiyo usiku na mchana waliisubiri mechi ya kwanza; nayo ikawa ni dhidi ya Everton, wale wale waliowavurugia hesabu za ubingwa, siku kadhaa kabla ya mwisho wa msimu uliopita.
Kadiri siku ya mwanzo wa msimu kwao ilivyokaribia, ndivyo washabiki, wachezaji na hata kocha walivyojawa hamasa ya kuanza na ushindi.
Robin aanza vibaya kwa mashetani wekundu
Baada ya kumpata nahodha wa zamani wa Arsenal, Robin Van Persie, basi wengi wakajijengea matumaini ya ushindi mkubwa, hata kama ule wa Fulham dhidi ya Norwich Jumamosi iliyopita wa 5-0.
Ni washabiki wachache walikuwa na wazo, hata kwa mbali, kwamba watoto wa Goodison Park wangeweza kuja kuwaaibisha mwanzo wa ligi.
Manchester walibabaika kwenye ulinzi na mashambulizi, licha ya kuwa na mfungaji bora wa mwaka jana, Van Persie na namba mbili, Wayne Rooney upande wao.
Na baada ya kosa kosa za mara kadhaa, Marouane Fellaini aliweza kuwahadaa washambuliaji, viungo, mabeki na hata golikipa – wote wakiwa golini kwa ajili ya kuokoa kona.
Walichelewa kuokoa na maji yakawa hayazoleki baada ya kumwagika, maana Fellaini aliweka ngoma kimiani kwa kichwa safi, akimwacha golikipa David Da Gea akishangaa bila hata kujirusha.
Hapo ndipo usiku ulipowakalia vibaya United, kwa sababu ilikuwa siku ambayo kila mmoja alitarajiwa azungumzie kuona ushirikiano mpya wa RVP na Rooney.
Naam, jinsi Shinji Kagawa anavyokitawala kiungo na kuwapelekesha puta vijana wa David Moyes au umwamba wa Nemanja Vidic aliyesemwa angerejea kwa nguvu baada ya miezi minane nje.
Haikuwa kati ya hayo yote, na hata alipoingizwa uwanjani RVP dakika ya 68 kwa tambo na watu kudhani ndio ushindi ungepatikana, tayari pambano lilishapata shujaa wake, kijana wa Kibelgiji aliyerithi mikoba ya Duncan Ferguson hapo Goodison Park.
Kocha Sir Alex Ferguson alionekana wazi kama simba aliyejeruhiwa, maana ni Everton waliotoa nao sare ya mabao 4-4, mechi ambao Man U walitakiwa washinde kabla ya ile ya mwisho.
Mchezaji wa Everton, Phil Jagielka alimsema mwenzake Fellaini mwenye urefu wa futi sita na inchi nne kwamba alikuwa kero kwa United.
Hii ni kwa sababu usiku ule aliwachambua alivyopenda Mashetani hao Wekundu, nao hawakupenda hali ile hata kidogo.
RVP naye alitoka uwanjani kichwa chini, huku baadaye Ferguson akilalamika kwamba wachezaji wenzake hawakumlisha mipira ipasavyo.
Aliingia na mpira wa kwanza aliogusa ilikuwa kona tasa aliyochonga, lakini baada ya hapo hakuna kashikashi yoyote aliyosababisha.
Ferguson akasema kwamba RVP anajulikana alivyo hatari akiwa kwenye maeneo fulani, kwani huwatesa mabeki, kwa hiyo ilibidi apewe mipira. Anasema Man U walicheza soka nzuri zaidi, lakini anakiri golikipa wake alihenyeshwa na washambuliaji wa Everton.
Nahodha wa United, Nemanja Vidic, anasema walicheza vizuri mpira, lakini Everton ni wagumu wakiwa kwao, na kwamba ukishatangulia kufungwa ni mzigo mzito kurudisha na kushinda. Anaamini mechi ijayo watafanya vyema, watakapowakaribisha Fulham Old Trafford.

Report

Tottenham Hotspur

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Robin van Persie started life at Manchester United with a defeat

Olympics 2012, London, Watanzania