in , , ,

REAL MADRID ILIJIBOMOA YENYEWE

Mwenendo wao umekuwa tofauti sana na msimu jana.

Msimu jana walikuwa na timu ambayo ilikuwa imara na kufanikiwa kuanza vizuri kwenye mbio za ubingwa wa La Liga.

Walianza na majeraha katika baadhi ya maeneo kwa kuwakosa wachezaji muhimu kama kina Kroos, Casemiro, Ronaldo.

Lakini walifanikiwa kukaa vyema katika mbio za ubingwa.

Msimu huu katika michezo 14 tayari wamekusanya alama 28, alama nane nyuma ya kiongozi wa ligi Barcelona.

*Nini tatizo la Real Madrid msimu huu?*

Msimu jana pamoja na kwamba walikabiliwa na majeraha kwa baadhi ya nyota wao, lakini kulikuwa na wachezaji ambao waliziba nafasi hizo na timu ikawa na uwiano.

Mfano mzuri ni Alvaro Morata , James . Hali iliyowafanya timu iwe na uwiano mzuri.

Baada ya wachezaji nyota kutoka kwenye majeraha , wakaingia kwenye timu. Kuna wakati timu ilikuwa inabanwa ilipokuwa inabanwa nje kulikuwa na wachezaji ambao walikuwa na uwezo wa kuleta mabadiriko makubwa kwenye mechi.

Mfano , pamoja na kwamba Alvaro Morata hakuwepa nafasi kubwa msimu jana lakini alifanikiwa kuhusika katika magoli 24 akiwa kama mshambuliaji mbadala.

Msimu huu kwenye benchi la Real Madrid hawana wachezaji mbadala ambao wanauhakika wa kubadilisha matokeo.

*Je mabeki wa Real Madrid wapo katika kiwango chao cha msimu jana?*

Hapana, kuna kitu kimepungua kuanzia kwa kiongozi Sergio Ramos , Carvajal, Marcelo.

Msimu jana Ramos alikuwa akihusika kufunga magoli muhimu sana. Lakini msimu huu imekuwa tofauti.

Upande wa kulia na kushoto mwa Real Madrid yalikuwa maeneo ambayo yalikuwa chachu kwa kiasi kikubwa kwenye mafanikio ya Real Madrid msimu jana, kwa sababu Marcelo, Carvajal walikuwa wakihusika kwa kiasi kikubwa katika kutengeneza nafasi nyingi tofauti na msimu huu.

Ukiliongelea eneo la ulinzi kushuka katika mchango wa kupatikana magoli huwezi kuacha eneo la kiungo.

Eneo hili pia lilikuwa nguzo muhimu. Casemiro alikuwa kiungo wa ukabaji lakini alikuwa akihusika katika upatikanaji wa magoli.

*Kushuka viwango kwa baadhi ya wachezaji muhimu inaweza ikawa tatizo?*

Ni jambo lililowazi baadhi ya wachezaji muhimu kama Kroos, Ronaldo , Benzema na majeraha ya mara kwa Mara ya Bale vimechangia kwa kiasi kikubwa kwa Real Madrid kuwa na wakati muhimu sana msimu huu

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

SIKU MBAYA ZAIDI ZINAKUJA ZINEDINE ZIDANE!

Tanzania Sports

Je ni : De Gea, Van Der Sar, au Peter Schmeichel?