in

PSPF wapeleka huduma mpya ya Bima ya Afya Majira, Mwananchi

Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu aliongoza ujumbe wa watendaji wakuu wa PSPF kutembelea vyumba vya habari vya magazeti ya Mwananchi na Majira, ikiwa ni utaratibu wa PSPF wa kutembelea vyombo vya habari kwa lengo la kufahamiana, kutolea ufafanuzi masuala mbalimbali na kupokea ushauri wa kuboresha huduma za PSPF.

Katika ziara hiyo iliyofanyika Desemba 2, 2015, Mkurugenzi wa PSPF aliongozana na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Bw. Gabrilel Silayo, Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bibi Neema Muro, Mkurugenzi wa TEHAMA, Bw. Andrew Mkangaa, Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi, Bibi. Costantina Martin, Afisa kutoka Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF, Bibi. Mathilda Nyallu na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Bw. Abdul Njaidi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Bw. Francis Nanai (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugezi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, baada ya kikao kazi kati ya Wahariri wa Mwananchi na Watendaji wa PSPF, kushoto ni Bw. Daniel Mwaijega Meneja Utawala Idara ya Habari na kulia ni Bibi. Matlida Nyalu Afisa wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF

Kituo cha kwanza cha safari hiyo ilikuwa katika ofisi za gazeti la Majira wachapishaji wa Gazeti la Majira na Business Times ambapo walikutana na watendaji wakuu wa kampuni hiyo.

Pia viongozi hao wa PSPF walitembelea ofisi za Mwananchi Communications zilizopo Tabata, ambapo walikutana na watendaji wakuu wa gazeti hilo. Katika maeneo yote watendaji wa PSPF walijibu maswali mbalimbali, walipokea ushauri na kutambulisha  huduma ya Bima ya Afya inayotolewa na PSPF kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

Meneja Mkuu wa Business Times Limited Bw. Aga Mbuguni (kushoto) akipokea machapisho mbalimbali ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF kutoka kwa Mkurugenzi mkuu wa Mfuko huo Bw. Adam Mayingu baada kikao cha watendaji wakuu wa taasisi hizo kilichofanyika Makao Makuu ya Business Times jijini Dar es Salaam.

“Lengo la ziara hizo ni kuwatembelea wenzetu wa vyombo vya habari kwa lengo la kufahamiana, kutolea ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali ya PSPF na kujifunza kutoka kwao jinsi ya kuboresha huduma zetu, pia kwa sasa tunatangaza huduma yetu mpya ya Bima ya Afya,hivyo tupo katika mpango wa kuwaelimisha waandishi wa habari ili na wao waweze kuelimisha umma juu ya mpango huo ambao ni mkombozi kwa watanzania wengi…huu ni mwendelezo kwani tulianza ziara hizi tangu mwaka jana,” alifafanua Bw. Mayingu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Vigogo FIFA wakamatwa

Tanzania Sports

Rushwa ya FIFA inatisha