Man United wapumua, Rooney out

*Chelsea safi, Arsenal, Liverpool sare

Ligi Kuu ya England imeendelea, ambapo Manchester United wamefanikiwa kuwapiga Wet Ham 2-1.

Hata hivyo, nahodha wao, Wayne rooney alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuwafungia bao la kwanza na la pili kufungwa na Robin van Persie.

West Ham walipata bao lao kupitia kwa Diafra Sakho kabla ya Rooney kupewa kadi nyekundu kutokana na kumchezea vibaya Stewart Downing.

West Ham walifunga bao la pili lililokataliwa na mwamuzi na kulalamikiwa na kocha Sam Allerdyce.

Rooney atakosa mechi dhidi ya klabu yake ya zamani ya Everton na pia West Brom na Chelsea.

Katika mechi nyingine Arsenal walikwenda sare ya 1-1 na mahasimu wao wa kaskazini ya Jiji la London wakati kwenye mechi ya kukata na shoka Liverpool walikwenda sare na wapinzani wao Everton.

Spurs walipata bao kupitia kwa Nacer Chadli wakatiArsenal walisawazisha kwa bao la Alex Oxlade-Chamberlain kwenye mechi iliyokuwa nzuri.

Liverpool wamesikitika kukosa ushindi, kwani Everton walifunga bao la kusawazisha dakika za mwisho kupitia kwa Phil jagielka katika dakika ya 90 baada ya Liverpool kudhani wangeondoka na ushindi kutokana na bao la nahodha Steven Gerard dakika ya 65 kwa mpira wa adhabu ndogo.

Katika mechi nyingine Chelsea walipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Aston Villa, yakifungwa na Diego Costa, Oscar na willian.

Mechi nyingine zilimalizika kwa Crystal Palace kuwafunga Leicester 2-0, Hull kufungwa 4-2 na Manchester City, Southampton kushinda 2-1 dhidi ya Queen Park Rangers na Sunderland kutoshana nguvu 0-0 na Swansea.

Posted under:  

Tags:  , ,

Comments