KAMATI YA BUNGE YA UKIMWI NA MADAWA YA KULEVYA YATEMBELEA MAKAO PSPF, WAFURAHISHWA NA MAFANIKIO YALIYOFIKIWA

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. George Yambesi (katikati) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya leo walipotembelea Makao Makuu ya PSPF, jijini Dar es salaam kuona namna mfuko huo ulivyopiga hatua katika kuboresha maisha ya wananchama wake na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi na madawa ya kulevya. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Lediana Mg’ongo na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu.

Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu akitoa taarifa kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya inayoshughulikia masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya walipotembelea Makao Makuu ya PSPF, jijini Dar es salaam.Kushoto ni viongozi wa Kamati hiyo Mhe. Diana Chilolo, Makamu Mwenyekiti na Lediana Mg’ong’o, Mwenyekiti wa kamati hiyo.

PSPF -6

Mwenyekiti wa Kamati Kamati ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya Mhe. Lediana Mg’ongo akisisitiza jambo wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wakati kamati anayoiongoza ilipotembelea makao makuu ya mfuko huo leo jijini Dar es salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF, Bw. George Yambesi na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu.

PSPF -7
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya Mhe. Lediana Mg’ongo akiongoza kikao cha wajumbe wa kamati yake na watendaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, jijini Dar es salaam. Mhe. Lediana Mg’ong’o ameupongeza uongozi wa mfuko huo kwa ubunifu na usimamizi mzuri wa mipango ya maendeleo inayowanufaisha wanachama wa mfuko huo.

Afisa Uhusiano Mwandamizi Mfuko wa Pensheni wa PSPF Bw. Bw. Abdul Njaidi akiwapatia fomu za kujiunga na Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSPF wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya walipotembelea PSPF jijini Dar es salaam. Mtanzania yeyote yupo huru kujiuga na mpango, akiwa katika sekta binafsi au sekta rasmi na haka akiwa mwanachama wa Mfuko mwingine wa hifadhi ya Jamii.

Wajumbe wa Kamati ya ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa mfuko wa Pensheni wa PSPF mara baada ya kuhitimisha ziara yao makao makuu ya mfuko huo jijini Dar es salaam.

Posted under:  

Tags:  , ,

Comments