in , ,

Fifa wamrejesha kitini Maigari

Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limemrejesha madarakani Rais wa Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF), Alhaji Aminu Maigari.

Tayari rais huyo ameingia ofisini baada ya kuwa ameondoshwa na serikali, Nigeria wakafungiwa na Fifa kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa, lakini amebakiza siku nane tu za utawala wake wa kipindi cha kwanza.

Maigari ameahidi kufanya kazi na wajumbe wote 13 wa Bodi ya NFF bila kubagua wale walioungana na kula njama za kumtupa nje ya ofisi yake. Amesema katika hilo hakuna mshindi wala aliyeshindwam bali wote wafanye kazi kwa ajili ya kukuza soka ya Nigeria.

Kipaumbele chake cha kwanza ni jinsi ya kuendesha uchaguzi huru na wa haki Agosti 26 jijini Warri. Agosti 14 Fifa ilitaka Maigari arejeshwe kwenye nafasi yake, lakini Kamati ya Utendaji ya NFF ikadai kwamba ilikuwa imemfungulia mashitaka kwa makosa kadhaa.

Hata hivyo, Ijumaa iliyopita, Waziri wa Michezo na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Taifa ya Michezo, Dk. Tammy Danagogo, alimtaka Maigari kurudi ofisini, ndipo mwalimu huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 58 aliporejea Jumatatu hii.

Mkurugenzi Msaidizi (Mawasiliano) wa NFF, Ademola Olajire alithibitisha jana kwamba Maigari amerejea madarakani rasmi na kwamba alifanya mkutano na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya NFF.

Alisema kwamba bodi imekuwa kitu kimoja baada ya kuweka kando tofauti zao kwa ajili ya maslahi ya soka ya Nigeria, ambapo Mwenyekiti wa Kamati ya Habari na Uenezi ya NFF, Chief Emeka Inyama, alieleza kwamba wanasonga mbele kuiopaisha Nigeria kisoka duniani.

“Sisi ni familia moja kubwa, kama ambavyo tumekuwa siku zote. Palikuwa na kutokukubaliana na kutoelewana kwa wiki kadhaa lakini Fifa imeshasafisha hali ya hewa na Serikali imeungana na Fifa hivyo tumeondoa tofauti zetu na sasa tunafanya kazi kuelekea uchaguzi ujao,” akasema Inyama.

Nigeria walikaribia kutupwa nje ya ulimwengu wa soka na Fifa, kutokana na serikali kuingilia shughuli za soka na mtifuano uliokuwapo ulisababisha baadhi ya masuala kutojadiliwa au kuchukuliwa hatua.

Mambo makuu mawili ni juu ya maandalizi ya Timu ya Taifa – Super Eagles kwa ajili ya mechi za kufuzu kwa kwa mashindnao ya 2015 lakini pia mazungumzo na wawakilishi wa Kocha Mkuu wa Super Eagles, Stephen Keshi aliyeachia ngazi, lakini NFF wanamsigi arudie kwenye kazi yake, kwani ndiye chaguo sahihi kwa Wanigeria.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Rwanda waeunguliwa Afcon

Arsenal, Besiktas ngoma mbichi