in , , ,

NILICHOKIONA KWENYE MECHI ZA UEFA


REAL MADRID VS BAYERN MUNICH.

Bayern Munich walifanya mechi ionekane wazi lakini refa alikuja kuziba
uwazi na kujenga ukuta ambao ƴulimwia ugumu Bayern Munich kupata
mlango wa kupitia.

Kuanza vizuri kwa Bayern Munich kulianza kuleta matumaini mapya juu ya
mchezo huu, kuna vitu vingi vipo na vitapotea baada ya muda mfupi ujao
pale Bayern Munich. Arjen Robben pamoja na Golikipa Manuel Neur ni
moja ya vitu vya thamani ambavyo kamwe huwezi kutamani muda wao wa
matumizi uishe mapema. Kwa kiasi kikubwa Manuel Neur alikuwa nguzo
muhimu kuifikisha katika muda wa nyongeza.

Robert Lewandowsky anaweza akawa na bahati kubwa sana na kuzifunga
timu za hispania maana katika mechi 5 alizokutana na timu za Hispania
amefanikiwa kuzifunga.

Lakini hii haikuwasaidia sana Bayern Munich kupita. Unaweza ukawa
umeangalia mabeki wa kushoto wengi katika maisha yako, lakini kwa muda
huu tuliopo Marcelo ni moja ya mabeki bora sana wa kushoto hasa hasa
anaposhambulia. Kwenye mechi hii alikuwa na msaada mkubwa sana kwenye
timu alipokuwa anaenda kushambulia.

Ronaldo anajua ameshazeeka , nguvu na kasi zimeanza kumtoka taratibu
mwilini mwake lakini ameanza kujua namna ya kucheza kulingana na umri
wake. Hana mambo mengi uwanjani kama kipindi cha ujana wake, yeye
anachoangalia ni namna gani nyavu zitakavyotingishika.

BARCELONA VS JUVENTUS.

Hakuna kitu kizuri ambacho nilikifurahia kwenye hii mechi kama ambavyo
refa aliufanya huu mchezo. Refa aliacha mpira uchezwe na yeye atazame
kwa umakini na kutoa maamuzi kitu ambacho hakikupoteza radha ya mchezo
kwani maamuzi yake yalikuwa na busara sana.

Barcelona waliingia uwanjani kwa ajili ya kutumia upande wa kulia wa
Juventus alipokuwa anacheza Dani Alves na Cuadrado. Neymar ndiye
alipewa ngao hii kitu ambacho kilimfanya aonekane ni mtu ambaye
alikuwa na hatari sana kwa upande wa Juventus.

Kuegemea sana upande wa kulia wa Juventus kulisababisha Juventus
wakose uwiano mzuri kati ya kushambulia na kuzuia, kwa kiasi kikubwa
madhara ya Cuadrado na Dani Alves yalionekana kwa kiasi kidogo sana.

Pamoja na Neymar kuonekana ni mtu hatari kwenye hii mechi lakini
mchezaji wangu bora kwa upande wa Barcelona alikuwa Gerrald Pique.
Gerrald Pique alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kukaba pamoja na kujenga
mawasiliano mazuri kati yake na Umtiti. Pamoja na hayo Gerrald Pique
alikuwa katika kiwango kizuri sana pindi alipokuwa anasaidia timu yake
kupandisha mashambulizi.

Pique alikuwa bora kwa upande wa Barcelona ila Pjanic alikuwa bora
kwenye mechi hii, alitimiza majukumu yake kwa kiwango kikubwa hasa
hasa kipindi cha kwanza.

Tunaweza tukawa tunawasifu sana mabeki wa Juventus kwa kujenga ukuta
imara wa timu , ƙlakini tukamsahau Alex Sandro. Alex Sandro alikuwa
mchezaji amabaye alikaba kwa kiasi kikubwa eneo la kati na kuna wakati
alikuwa anaisaidia timu kupanda mbele.

Ni mapema sana kusema Messi ameisha ila kwa mechi ya jana hakuwa na
mchezo mzuri, alikosa umakini ambao ulimsababisha akose nafasi za
kufunga za wazi.

MONACO VS BORRUSIA DORTMUND.

Mechi ilikuwa imeshaisha Ujerumani, huku Ufaransa Monaco walitakiwa
kukamilisha kazi ndogo kati ya kubwa ambayo waliifanya Ujerumani. Kitu
kizuri ambacho Monaco walikifanya na kuwasaidia kwa kiasi kikubwa ni
namna ya wao walivyokuwa wanashambulia kwa kushtukiza.

Timu yote ilipokuwa inaenda kushambulia kulikuwa na ushirikiano mkubwa
sana hata mabeki wa pembeni kwa pamoja walikuwa wanaisaidia timu
kupanda kushambulia kwa pamoja.

Kitu kizuri ambacho Monaco walionekana tofauti na mechi ya Man City ni
kwamba kwenye mechi hii ukuta wao ulikuwa imara sana na mabeki
walikaba vizuri sana tena kwa nidhamu kubwa .

Falcao anaongeza ukomavu kwa wachezaji wadogo wanaomzunguka. Kina
Mbappe wanaonekana wamekomaa kulinganisha na umri wao.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

TUIPUMZISHE TFF MZIGO , TUINGIE WOTE VITANI

Tanzania Sports

HILI LA MAANDAMANO YA SIMBA WANAFANYA KWENYE TAA NYEKUNDU