in , , ,

NILICHOKIONA KWENYE MECHI YA AZAM NA SIMBA

Kuwaanzisha Stephano, Frank Domayo na Himid Mao kwa wakati mmoja eneo
la katikati kulikuwa na maaana moja kubwa sana kwa Azam.

Viungo wote hawa watatu wana asili Kubwa ya kukaba na ndogo ya
kushambulia. Hii iliifanya safu ya eneo la katikati mwa uwanja kuwa
imara zaidi.

Tatizo lililokuja kuisumbua Azam ni kwamba, Kuwaanzisha Singano na
Mahundi katika eneo la pembeni ilikuwa ni kuwapa majukumu wao kutoa
huduma ya mipira kwa Bocco huku wakiwa wanaichukua mipira katikati
wakitokea pembeni mwa uwanja.

Tatizo lililokuja kuwanyima wao kutokutoa huduma nzuri kwa Bocco ni
kwamba, mabeki wa pembeni wa Simba yani Bukungu pamoja na Mohamed
Hussein walikuwa imara kuzuia mijongee ya kina Mahundi na Singano.

Ndiyo maaana kipindi cha kwanza Bocco alipata mipira michache sana
akiwa eneo la Kumi na nane ya Simba.

Kitu kingine ambacho kilisababisha Azam washindwe kufanya mashambulizi
kupitia pembeni ni kwamba Erasto Nyoni hakuwa anapandisha vizuri
mashambulizi ya timu.

Heka heka uwanjani

Kwa upande wa Simba kwa kipindi cha Kwanza, Muda mwingi walitumia
kucheza katika eneo lao zaidi, hii ni kutokana na Azam kujaza viungo
wengi kwenye eneo la katikati, kitu ambacho kilikuwa kigumu kwao
kupenyeza mipira kuwafikia kina Atanas na Luzio.

Na hii ilipelekea katika kipindi cha kwanza, washambuliaji wa Simba
kutokupata mipira mingi katika eneo lao. Hii ni kwa sababu mpira kwa
kiasi kikubwa ulichezwa katika eneo la kiungo zaidi.

Kipindi cha pili kilikuja na mabadiliko makubwa sana kwa Simba.

Mara baada ya wao kuona ni ngumu kwao kupitia katikati mwa uwanja,
wakaamua kucheza direct football (mpira wa moja kwa moja), pia wakawa
wanacheza kwa kupitia pembeni.

Heka heka angani (Picha zote kwa hisani ya @SalehJembe)

Kitu ambacho kilisababisha Simba wapate mipira mingi katika eneo la
kumi na nane la Azam.

Kitu kilichowagharimu Simba.Kwanza pengo la Bukungu,baada ya
Bukungu,kuumia waliamua kuchezesha mabeki watatu.

Na kuwekeza zaidi kwenye kushambulia ambapo walishambulia bila
tahadhari na ndipo hapo kitu cha pili kilichowagharimu kinapokuja.

Baada ya Simba kuanza kushambulia, Azam walitulia nyuma wakawa
wanakaba kwa nidhamu.

Kikosi cha SImba Sports Club

Utulivu ambao uliwasaidia hata wao kufanya shambulizi la kushtukiza
ambalo lilitokea eneo la kulia mwa Uwanja, eneo ambalo Bukungu
alikuwa anacheza awali. Na ndipo hapo Goli lilipozaliwa.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

KIPI WAKIFANYE SIMBA ILI WASHINDE MECHI DHIDI YA AZAM?

Tanzania Sports

SABABU ZA KWANINI LIVERPOOL WATASHINDA DHIDI YA CHELSEA.