in , ,

Neymar arudishwa nyumbani

neymar

*Afungiwa mechi nne, bado kashfa ya kodi

Nyota wa Brazil, Neymar, aliyetarajia kung’ara kwenye michuano ya Copa America ameishia kwa hasara kubwa, baada ya kufungiwa mechi nne.

Neymar (23) hataonekana tena kwenye michuano hiyo kwani anarudishwa nyumbani kutokana na utovu mkubwa wa nidhamu alioonesha, akapewa kadi nyekundu walipofungwa na Colombia.

Mshambuliaji huyo wa Barcelona alikuwa amefungiwa mechi moja tu baada ya kitendo chake cha kumpiga mchezaji wa Colombia, Pablo Armero kwa mpira, ambapo angekosa tu mechi ya mwisho ya makundi dhidi ya Venezuela Jumapili hii.

Hata hivyo, Shirikisho la Soka la Amerika Kusini limepitia upya shauri hilo na kuongeza adhabu. Alifanya kitendo cha kipuuzi kwani kipenga cha mwisho kilishapulizwa alipompiga Armero kisha akaonekana akimpiga kichwa mchezaji mwingine, ikiwa ni hasira kwa kufungwa wakati wote walikuwa na muda sawa dimbani.

Mchezaji wa Colombia, Carlos Bacca, ambaye pia alipewa kadi nyekundu kwa kulipiza kisasi amezuiwa kukaa benchi la ufundi kwa mechi mbili na wachezaji wote wana haki ya kukata rufaa. Bacca alimchota mtaka Neymar.

Mbrazili huyo tayari alikuwa ameshaoneshwa kadi ya njano mapema kwenye mechi dhidi ya Colombia kwa mchezo mbaya.

Katika fainali za Kombe la Dunia nchini mwake mwaka jana, Neymar alilazimika kuondoshwa kwenye mashindano baadaya kuvunjika kifundo cha uti wa mgongo, baada ya kugongwa kwa goti na mchezaji wa Colombia, Juan Zuniga ambaye hata hivyo hakuadhibiwa.

Imeonekana ni mwendelezo wa mkosi kwa mchezaji huyo katika michuano ya kimataifa.

Hivi sasa Neymar atarejea nyumbani ambako anakabiliwa na shauri la kukwepa kulipa kodi, ambapo uchunguzi unaendelea.

Waendesha mashitaka wanasema kwamba wameshitushwa na mtiririko wa kiasi kikubwa cha fedha kwa Neymar katika kampuni ya wazazi wake, ambapo maofisa wa kodi wanasema kwamba hazikulipiwa kodi.
Akaunti hizo zimefuatiliwa kati ya 2011 na 2014 ambapo kiasi kinachodaiwa kutolipiwa kodi ni zaidi ya pauni milioni 24.

Mchezaji mwenzake wa Barcelona, Lionel Messi naye anakabiliwa na shauri kama hilo lakini wachunguzi wa mambo wanasema atapona kwa kulipa faini ikiwa atatiwa hatiani

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Trapattoni, Domenech waitaka Ivory Coast

KASHFA YA MLUNGULA FIFA: