in

Motema Pembe: Tutaifanya Simba daraja

Timu ya DC Motema Pembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliwasili jijini Dar es Salaam jana saa 10 jioni tayari kwa mechi yao ya kesho huku wakijigamba kwamba wataifanya Simba daraja la kuelekea katika hatua ya makundi ya mashindano hayo ya Kombe la Shirikisho.


Akizungumza muda mfupi baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, kocha wa timu hiyo, Joseph Mukeba Mulamba, alisema kuwa timu yake imejiandaa vyema kuikabili Simba na inaamini kwamba itashinda mechi ya kesho na ile ya marudiano itakayochezwa kwao Kinshasa wiki ijayo.

Mulamba ambaye alirejeshwa kwenye kikosi cha timu hiyo mapema Jumanne alisema kwamba wamekuja Tanzania kushinda na kuionyesha Simba kwamba wao wanafahamu kucheza na si kufanya jambo jingine.

“Tumekuja kuwaonyesha maajabu hapa nyumbani kwao, mechi na Simba ni njia ya kufika mbali katika mashindano haya ya Afrika,” alisema kocha huyo.

Aliongeza kuwa wachezaji wote 18 waliokuja nao wako katika hali nzuri na walitumia mazoezi ya wiki moja jijini Kigali nchini Rwanda kujifua kwa ajili ya kuikabili Simba.

“Tumebanwa na mechi za ligi ya nyumbani, hatujacheza mechi hata moja ya kujipima ila zile zile za ligi zinatosha kutuimarisha na kuonyesha uwezo wetu,” Mulamba aliongeza.

Alisema kwamba wao wanauzoefu na mechi za kimataifa na wanaamini kwamba ushindi wa kesho utawaweka katika nafasi nzuri ya mechi ya marudiano.

Naye nahodha wa timu hiyo, Glady Bokese, alisema kwamba wanaiheshimu Simba lakini wamekuja nchini kwa kazi moja tu ya kupambana na kuibuka washindi.

Bokese alisema kwamba licha ya rekodi nzuri iliyonayo Simba kwenye mashindano, wao wanataka pia kuwaondoa wapinzani wao na kucheza hatua ya makundi.

“Nilikuja na timu ya taifa nikashinda, sasa pia niko na klabu lazima tutashinda pia,” alijigamba nahodha huyo.

Kocha wa Simba, Moses Basena, alisema kuwa mechi ya kesho ni ngumu kwa sababu wachezaji wa Afrika wote wanafahamiana na kilichoko ni kuhakikisha wanatumia nafasi watakazopata kufunga.

Basena alisema kwamba haitaji kuwapeleleza wapinzani na anahitaji kuhakikisha kila idara kwenye timu yake inaelewa inatakiwa ifanye nini uwanjani.

Mechi hiyo ya kwanza kati ya Simba na DC Motema Pembe itaanza saa 9:30 alasiri kesho kwenye uwanja wa Taifa na watarudiana kati ya Juni 17 na 19 mjini Kinshasa.

CHANZO: NIPASHE

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Loading…

0

League agrees to new Uefa financial regulations

Tanzania: Sports Budget Draws Harsh Reaction