in

Manchester United taabani

Alex Telles

Manchester United wapo katika hali mbaya, baada ya kukubali kichapo cha mabao sita kutoka kwa Tottenham Hotspur kabla ya mapumziko ya kupisha michuano ya kimataifa.

Wachezaji wake wanaonekana kutokuwa na utimamu wa mwili wala utulivu wa akili, huku ingizo jipya la Januari katika Bruno Fernandes nalo likipoteza matumaini makubwa ya wengi baada ya kuonekana kupwaya.

Inaelezwa sasa kwamba wakuu wa Old Trafford wana hofu juu ya mwenendo wa klabu na kuna watu wa nje wanaona kwamba Mashetani Wekundu hawa wanapoteza tu fedha na wakati kwa kuwa na watu wasiotakiwa.

Ole Gunnar Solskjaer – kocha wao na mchezaji wao wa zamani kwenye kiungo ana wakati mgumu, maana hakupata hata mmoja wa wachezaji aliokuwa amepanga kuwasajili kiangazi hiki hadi dirisha linafungwa Jumatatu iliyopita.

Walikuwa wanahitaji mabeki, viungo na hata mshambuliaji lakini wote waliopangwa, akiwamo mshambuliaji Jadon Sancho wa Borussia Dortmund hawakupatikana, wakaishia kubabatiza na kumpata mchezaji huru Edinson Canani mwenye umri wa miaka 33 anayeelekea kustaafu soka na ambaye hukumbwa na majeraha ya mara kwa mara.

OLE

Inaelezwa kwamba wakuu wa Manchester wameingiwa wasiwasi na hali ya kiakili na mwili ya Fernandes aliyeng’ara sana na aliyetokea kuwa mpiga penati wao, lakini ilibidi apumzishwe baada ya kipindi cha kwanza walipocheza na Spurs, maana licha ya kufunga penati awali, alitokea kuchoka na kushindwa kabisa kuumudu mchezo.

Kiungo huyu raia wa Ureno alisajiliwa kutoka Sporting Lisbon na akawafufua United, wakawa wazuri tangu Januari hiyo, lakini sasa anaonekana kupwaya. Taarifa zilizonukuliwa na gazeti la michezo la Ureno liitwalo ‘O Jogo’, United wameanza kuwa na wasiwasi na hali ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.

United walipoteza mechi dhidi ya Spurs kwa kufungwa 6-1 Jumapili kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford. Hiki ni kipigo kikubwa na cha kihistoria, wakati huu ambapo United wamefikisha matumizi ya pauni bilioni moja kwenye usajili wa wachezaji tangu kustaafu kwa Sir Alex Ferguson, lakini hapakuwapo na matokeo chanya kutoka kwao.

Fernandes alitajwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya England (EPL) kwa mwezi Februari na Juni mwaka huu, ambapo mabao yake na usaidizi kwa mabao ulikuwa muhimu kwa klabu kufanikiwa kumaliza ndani ya nne bora.

Baada ya kuchezea kichapo hicho cha Jumapili, Fernandes aliwaomba radhi washabiki kupitia akaunti yake ya Instagram akisema; “tunaomba radhi kwa washabiki wote kwa kipigo hiki kikubwa nyumbani. Ni muda wa kuinamisha vichwa vyetu, kutafakari na kujiandaa kufanya zaidi kwa ajili yetu, kwa klabu na washabiki.”

Inadaiwa kwamba Fernandes anaweza kuwa amechoka kutokana na kucheza mfululizo lakini pia inawezekana kuwa ni mwendelezo wa kawaida wa kushuka viwango kwa majina makubwa yanayosajiliwa Old Trafford, kama ilivyokuwa kwa akina Angel di Maria na wenzake.

DAPamoja na wasiwasi juu ya Fernandes, inaelezwa kwamba hatma ya kocha Solskjaer nayo ipo shakani kuitokana na timu kuonekana kukosa mfumo unaoeleweka, kushindwa kupeana pasi za uhakika, kulinda lango na kutikisa nyavu licha ya kuwa na wachezaji wazuri kama akina David de Gea, Paul Pogba na wenzake.

Kuna taarifa kwamba Man U wanafikiria kufanya mazungumzo na kocha wa zamani wa Spurs, Mauricio Pochettino ambaye kwa sasa hana kazi na alipata kuwindwa na Barcelona. United wameambulia alama tatu tu katika mechi tatu, baada ya kupoteza mechi ya kwanza dhidi ya Crystal Palace na kuwashinda Brighton kwa mbinde.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
wachambuzi wa soka

Korona Inavyoendelea kuwaadhibu Wachambuzi

ureno

Hispania, Ureno nguvu moja