Man U washinda, kadi yakosewa

Manchester United wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Sunderland kwenye mechi ambayo Wes Brown alipewa kadi nyekundu badala ya John O’Shea.
Huu ni ushindi wa 11 katika mechi 14 za United, ambapo nahodha Wayne Rooney alifunga bao la kwanza katika mechi tisa alizowachezea Man U.

Sunderland walijitahidi kuwazuia Manchester lakini ilipofika dakika ya 66 walikubali bao la penati ya Rooney na dakika ya 84 akafunga jingine.
Sunderland, maarufu kwa jina la Paka Weusi wamebaki alama tatu juu ya mstari wa kushuka daraja. Penati ilitolewa baada ya O’Shea kumchezea rafu Radamel Falcao lakini aliyepewa kadi nyekundu akawa Brown kutoka kwa mwamuzi Roger East.

image

Ushindi huo umewarejesha United kwenye nafasi ya tatu nyuma ya Chelsea wanaoongoza na Man City ambao ni mabingwa watetezi.
Mwamuzi wa akiba alikuwa Martin Atkinson aliyelalamikiwa kwa jinsi alivtochezesha mechi baina ya Chelsea na Burnley iliyoisha kwa sare wiki iliyopita.

Kwenye matokeo mengine Jumamosi hii, West Ham walipokea kichapo cha 3-1 kutoka kwa Crystal Palace, Burnley wakafungwa na Swansea 1-0, Newcastle wakawashinda Aston Villa kwa 1-0 kama Stoke walivyowazidi nguvu Hull na West Bromwich Albion kuwagagadua Southampton.

Jumapili hii ni kipute baina ya Liverpool wanaowaalika man City huku Arsenal wakiwa wenyeji wa Everton.

Comments