Man City, Arsenal raha

Mbio za ubingwa wa England zimeendelea kunoga, ambapo wanaoshika nafasi za pili na tatu bado wanafukuzana.
Huku Chelsea wanaoongoza kwa pointi 64 wakiwa wametulia kusubiri mechi ya Jumapili, mabingwa watetezi, Manchester City wamepata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya West Bromwich Albion.
City wakiwa nafasi ya pili kwa pointi zao 61 bado wanakabwa na Arsenal ambao wamefikisha pointi 60 baada ya kuwafunga Newcastle 2-0.

Katika mechi ya Man City, inadaiwa kwamba mwamuzi Neil Swarbrick alimpa kadi nyekundu mchezaji ambaye siye wa West Brom, huku mshambuliaji mpya wa City, Wilfried Bony akifunga bao la kwanza tangu ajiunge Etihad.

Fernando wa City alifanya kazi ya kihistoria kw akufunga bao la 1,000 katika Ligi Kuu ya England (EPL) kwa City.
Mabao ya City yalifungwa na Bony, Fernando na David Silva. Mchezaji wa West Brom aliyetolewa kwa makosa ni Gareth McAuley badala ya Craig Dowson aliyemchezea Bony rafu.

msimamo

Kwa upande mwingine, Arsenal waliendelea kuchekea ushindi baada ya kuwapiga Newcastle 2-1 kwa mabao ya Olivier Giroud katika dakika ya 24 na ya 28, ambapo Mfaransa huyo anaonekana kurudi kwenye kiwango.

ousa Sissoko aliwafungia wageni bao la kufutia machozi dakika ya 48. Huu ni ushindi wa sita mfululizo kwa Arsenal katika EPL na wanabai pointi moja tu nyuma ya Man City.
Matokeo mengine yameshuhudia Aston Villa wakilala kwa Swansea 1-0, Sounthampton wakiwafunga Burnley 2-0, Stoke wakilala 2-1 kwa Crystal Palace, Tottenham wakishinda 4-3 dhidi ya Leicester na West Ham wakipumua 1-0 kwa Sunderland.

Comments