in , ,

Makocha wanaofaa kuchukua nafasi ya JOSE MOURINHO

Makocha wanaofaa kuchukua nafasi ya JOSE MOURINHO

Baada ya misimu miwili akiwa na Manchester United, Jose Mourinho amefukuza kazi hapo Jana. Na hii inakuwa ni mwendelezo wa matokeo mabovu kwa kila msimu wake wa tatu.

Ameondoke Manchester United, anakuwa kocha wa tatu kufukuzwa tangu Sir Alex Ferguson kuondoka ndani ya miaka mitano iliyopita. Je, ni makocha wapi wana nafasi kubwa kuchukua nafasi yake?

RYAN GIGGS

Miongo miwili imetumika kuhakikisha miguu ya Ryan Giggs ikitumikia nyasi za Old Trafford. Ni moja ya wachezaji bora kuzalishwa katika kikosi cha Manchester United.

Na ni vigumu sana kumuacha kwenye kikosi bora cha muda wote cha Manchester United. Ametumia muda mwingi akiwa ndani ya hii klabu hii ndiyo nguzo kubwa ambayo anaweza kuitumia kwa ajili ya kukifundisha kikosi cha Manchester United.

Anajua utamaduni wa Manchester United kwa sababu ameuishi kwa muda mrefu, maisha yake ya mpira yaliumbwa kwa damu inayoitwa Manchester United.

Ryan Giggs aliwahi kufundishwa na Sir. Alex Ferguson kwa muda mrefu sana. Tangu Sir. Alex Ferguson aondoke, Manchester United imepoteza utambulisho wake wa kucheza mpira, Ryan Giggs ana nafasi kubwa sana ya kurudisha utambulisho wa timu kwa sababu aliishi ndani ya maisha ya Sir. Alex Ferguson kwa muda mrefu.

LAURENT BLANK

Wakati Manchester United inamfukuza Louis Van Gaal , Kocha ambaye alikuwa anatajwa sana kuchukua nafasi yake ni Laurent blank , Kocha wa zamani wa PSG. Sababu kubwa ambayo inanifanya nimuone kama ni kocha ambaye anaweza kuja kuifundisha Manchester United ni mahusiano mazuri aliyonayo na viongozi wa Manchester United.

A. CONTE

Wakati yupo Chelsea na Juventus, kitu ambacho kilimsababisha aondoke ni yeye kutopewa pesa nyingi katika dirisha la usajili ili kununua baadhi ya wachezaji ambao anaona wanafaa.

Manchester United ni aina ya timu ambayo hutumia fedha nyingi kwenye usajili, kwa hiyo kama atakuja basi itakuwa nafasi nzuri kwake yeye na Manchester United kufanya vizuri.

Conte ameishi England miaka miwili na akafanikiwa kuchukua vikombe viwili (Ligi kuu ya England pamoja na FA CUP).

Hii inaonesha dhahiri kuwa hatokuwa mgeni kwenye soka la England kwa sababu analijua kwa asilimia kubwa hivo itamsaidia kuirudisha Manchester United.

ARSENE WENGER

Hana kazi kwa muda mrefu sasa, miezi sita ishapita akiwa nje ya uwanja. Arsene Wenger alichokuwa anahitaji ni kupumzisha akili kwa muda.

Hakuwa ameishiwa kama kocha, alifanya kazi kubwa kwa muda mrefu bila kupumzisha akili. Ashapata huo muda baada ya kutoka Arsenal. Naamini kwa sasa yupo tayari kuchukua majukumu mengine ya kufundisha tena klabu kubwa.

Manchester United ya Jose Mourinho ilikosa nguvu kwenye chumba cha kubadilishia nguo, hakukuwa na uongozi ambao ni mzuri ndani na nje ya vyumba vya kubadilishia nguo.

Kwa hiyo Arsene Wenger anauwezo mkubwa wa kurudisha hii hali ambayo ilipotea kwa huo muda. Pia ametumia muda mrefu akiwa kwenye soka la England , analijua kwa kiasi kikubwa hivo hatokuwa mgeni wa soka hili.

Aina ya mpira ambao anacheza ni wa kushambulia. Aina ambayo walikuwa wameikosa kwa muda Manchester United.

MAURICIO POCHETTINO

Moja ya kitu ambacho Sir.Alex Ferguson alikuwa anakifanya ni yeye kupandisha wachezaji vijana na kuwapa nafasi kubwa sana kwenye kikosi chake.

Hiki kitu Mauricio Pochettino anacho, ameitoa Tottenham Hotspurs kwenye timu za kati mpaka kuwa kwenye timu ambayo inauwezo wa kugombania ubingwa.

Ametumia asilimia kubwa vijana ambao aliwapandisha na kuwaamini. Pia Mauricio Pochettino anacheza mpira wa kushambulia na wa kuvutia kitu ambacho ni hitaji kubwa la Manchester United.


Zinedine Zidane

Ametumia miaka miwili na kupata vikombe Tisa ndani ya klabu ya RealMadrid, inawezekana alikuwa na aina ya wachezaji ambao ni wakubwa.

Lakini alifanikiwa kuishi nao, wakawa na morali ya kupigana. Hiki ndicho kitu ambacho Manchester United wanakosa. Hakuna nguvu kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, wachezaji hawana morali na hawapigani kwa kiasi kikubwa.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Serengeti boys

Tumkumbuke MALINZI na SERENGETI BOYS yake

Tanzania Sports

Natamani hadithi ya Zidane ifunikwe na jalada la Ole Gunnar Solskjær