Liverpool mambo magumu

 

 

Liverpool wameendelea na hali duni dimbani baada ya kukubali kichapo cha 1-0 kutoka kwa Hull wanaopambana ili wasishuke daraja.

 

Alikuwa Michael Dawson aliyewainua washabiki kwa kufunga bao dakika ya 37, likiwa ni lake la kwanza tangu Januari 2013.

 

Wakati Liverpool wameachwa kwa pointi saba kufikia timu nne bora zitakazofuzu kwa Ulaya, Hull wameongeza pengo la pointi nne kati yao na timu tatu zinazotakiwa kushuka daraja.

 

Liverpool walishindwa kutengeneza nafasi, ambapo Mario Balotelli aliyepewa fursa ya kurudisha umahiri wake aligusa mpira mara moja tu ndani ya dakika 20 kabla ya kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Rickie Lambert dakika ya 65.

 

Liverpool wenye pointi 58 wapo nyuma ya Manchester United waliojikusanyia pointi 65, Arsenal wenye 67 sawa na Manchester City huku Chelsea wakiongoza kwa pointi 77.

 

Man City, United na Liver wamecheza mechi moja zaidi ya Arsenal na Chelsea na Liver wanalingana kwa pointi na Tottenham Hotspur wanaoelekea kupigania kucheza Ligi ya Eurpopa pamoja na Southampton wenye pointi 57.

 

Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers amesema wachezaji wake wataendelea kupambana ili kumaliza msimu vyema.

 

Burnley wamebaki mkoani mwa ligi wakiwa na pointi 26, QPR wakifuatia wakiwa nazo 27 na Sunderland wanazo 30. Leicester bado wapo hatarini kwani wana 31 na Aston Villa wanazo 32, mbili pungufu ya Hull.

 

Comments