in , , ,

Kwanini tumeona ‘Extra time’ nyingi Kombe la dunia

Kuna swali moja tu; Kwanini michuano hii kumekuwa na ‘Extra Time’ kibao?

Katika michuano hii tumejionea rekodi mbalimbali, lakini kubwa zaidi Algeria wamefanya jambo moja zuri sana katika ulimwengu wa soka la Afrika.

Ujerumani walilipa kisasi cha mwaka 1982 kufungwa bao 1-0 na kikosi cha Algeria cha akina Djamel Zidane. Tukiacha hilo kuna hili la wachezaji wanaotokea benchi na kufunga mabao ya kusisimua.

Juzi tulishuhudia bao la Kevin De Bruyne akiifungia bao muhimu Ubelgiji mara baada ya kuingia uwanjani kuchukua nafasi ya mshambuliaji Romelu Lukaku.

Lakini fainali za Kombe la Dunia mwaka huu zimeshuhudia mabao 29 ya wachezaji waliotokea benchi. Watunza rekodi wa mtandao wa Opta wameonesha kuwa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 zimetia fora kwa kuweka rekodi ambapo wachezaji waliotokea benchi wamefunga mabao 29.

Hii ni tofauti na fainali za mwaka 2006 ambapo wachezaji hao walifunga mabao 23, mwaka 2002 ( 21), mwaka 1990 (20) na mwaka 1982 mabao 16.

Opta wamesema kuwa fainali za mwaka huu zimevunja rekodi ya mwaka 2006 ambapo wachezaji waliotokea benchi walifunga mabao 23, lakini fainali za Brazil zimeshuhudia mabao 29, ikiwa ni sita mabao zaidi.

Wachezaji waliochangia kuvunja rekodi hiyo ni Haris Seferovic (Uswisi), Miroslav Klose (Ujerumani), Silvestre Varela (Ureno), na Andre Schurrle (Ujerumani).

Turudi kwenye swali la msingi, ambapo Brazuca imeshuhudia mechi ikienda hadi extra time. Mechi kati ya Uholanzi v Mexico haikufika Extra time.

Mechi kati ya Nigeria v Ufaransa haikufika Extra Time. Lakini mechi kati ya Brazil v chile, pale mjini Fortaleza ilikwenda hadi Etra Time na matokeo yakawa 1-1.

Ilibidi mwamuzi Howard Webb aendelee hadi kwenye hatua ya matuta ili kumpa mshindi. Hii ilikuwa mechi ya kwanza ya raundi ya pili. Pia ni mechi ya kwanza kumalizika kwenye Extra Time.

Mechi ya pili ni kati ya Costa Rica v Ugiriki ambayo ilikwenda hadi hatua ya matuta ndipo mshindi akapatikana. Mechi ya tatu ya raundi ya pili ilikuwa ya Ujerumani v Algeria ambayo ilimalizika wakati wa Etxra Time kwakuwa wajerumani walipata mabao mawili kabla ya filimbi ya mwisho.

Mechi ya nne kwenda Extra Time ilikuwa kati ya Argetina v Uswisi iliyochezwa mjini Sao Paulo. Kikosi cha Alejadro Sabella kilipata bao la ushindi dakika chache kabla ya kumalizika kipindi cha mwisho cha Extra Time lililofungwa na Angel Di Maria.

Mchezo wa mwisho ulioingia Extra Time ni kati ya Marekani v Ubelgiji uliochezwa kwenye uwanja wa Arena Fonte Nova mjini Sao Paulo. Sasa kwanini tumefika hapo?

Kwanza kabisa tukiangalia timu zote zina makosa mbalimbali ya ulinzi na ushambuliaji. Hadi sasa hakuna ‘forward’ mwenye makali, sababu hakuna aliyepachika mabao mengi.

James Rodriguez ni kiungo mshambuliaji, siyo mshambuliaji kamili. Fred Chaves, Jo, Romelu Lukaku, Mario Balotelli, Sergio Aguero, Karim Benzema na washambuliaji wengine hakuna mwenye makali hadi leo.

Pengine tunaweza kusema safu ya ulinzi zimekuwa imara, lakini tukubali pia kuwa baadhi ya makipa wa timu hizo zilizofika extra time ni wazuri mno.

Keyla Navas wa Costa Rica umahiri wake siyo wa kutiliwa shaka kwa wale wanaotazama La Liga akiwa na klabu ya Levante. Makipa wa timu zilizofika Extra time wameonesha umahiri mkubwa huku safu za ulinzi zikiwa na makosa yanayofanana.

Brazil ilijifunga dhidi ya Croata kupitia Marcelo da Silva. Kosa hilo hilo limejirudia kwa mabeki wa Ujerumani ingawa hawakujifunga dhidi ya Algeria.

Nigeria ilifungwa kwa makosa ya aina hiyo lakini Vincent Enyeama alikuwa bora uwanjani. Timu kubwa zina matatizo, timu ndogo zinatumia faidia ya matatizo hayo kujitutumua.

Lakini ukweli mechi zote zilizokwenda extra time na walioshinda walitumia uzoefu, hakukuwa na mbinu mbadala za makocha. Kingine ni kiwango cha ushindani kinachooneshwa na makocha wao, mfano Algeria, Colombia, na Costa Rica.

Huwezi kushinda mechi kama hujui kuzuia. Huwezi kushinda mechi kama washambuliaji hawafungi. Huwezi kushinda mechi kama golikipa siyo imara.

Kwahiyo tumefika kwenye kiwango kikubwa cha ushindani kuanzia makocha wa timu ndogo hadi kubwa. Makocha wa timu kubwa wametegemea uzoefu, hawajaonesha ubora wa kiwango cha juu. Bado viwango vya wachezaji si vya juu. Tuseme michuano hii imekuwa bora kwa makipa na ndiyo wameonesha viwango vya juu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Barca, Liver wakubaliana ya Suarez

Argentina wawazidi Ubelgiji