in ,

KWA HILI, YANGA WANA HAKI YA KUPEWA POINT(S)

Yanga

Jana kulikuwa na mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara katika uwanja wa
Sokoine kati ya Mbeya City na Yanga.

Katika mchezo huo ulimalizika kwa timu zote kutoka sare ya goli 1-1,
kuna mengi yaliyotokea ikiwemo vurugu ambazo zilianzishwa kwenye
mchezo huo.

Lakini kuna tukio moja ambalo lilitokea katika mchezo huo ulipokuwa
unaelekea mwishoni.

Kabla Mbeya City walikuwa tisa (9) kwani dakika ya 70 mchezaji Bakari
Malima wa Mbeya City alipewa kadi nyekundu.

Na katika dakika ya 96 mwamuzi wa akiba alionesha kibao cha
mabadiliko, Eliud Ambokile jezi namba kumi (10) alitakiwa apumzike
na mchezaji mwenye jezi namba kumi na sita (16) alitakiwa aingie.

Wakati mwamuzi wa akiba akionesha kibao cha mabadiliko Eliud Ambokile
alikuwa anapatiwa huduma ya kwanza nje ya uwanja alipata majeraha
kidogo. Baada ya kumaliza kupatiwa huduma ya kwanza aliomba kuingia na
mwamuzi wa kati akamruhusu kuingia.

Na kufanya idadi ya wachezaji wa Mbeya City ndani ya uwanja kuwa
kumi(10) badala ya tisa (9).

Hivo Mbeya City walinufaika na mabadiliko hayo kwa takribani dakika
moja. Yanga kwenye hili wana haki ya kulalamika na wanahaki ya
kusikilizwa na kupewa haki yao stahiki.

Kutojua sheria sio utetezi kwenye kesi yoyote ile, kosa limetokea
hakuna bahati mbaya kwenye kosa na hii inanikumbusha tukio ambalo
liliwahi kutokea hapa hapa Tanzania msimu wa 2014/2015.

*Kagera sugar vs Rhino rangers* mchezaji wa Rhino alipewa kadi
nyekundu hivyo Rhino waliimuingiza mchezaji mwingine, katika mazingira
ambayo aliyetokewa hakujua hivyo wakaendelea kucheza wakiwa na
wachezaji kamili 11 uwanjani.

Mechi ikiisha kwa sare ya 0-0. Baada ya Mechi TFF waliamua kuipa
Kagera goli tatu na point tatu kwa kosa lifuatalo.

Rhino wamevunja sheria kwa kuchezesha wachezaji 12 katikati kwa wakati
Mmoja uwanjani bila kufanya mabadiliko, na ni kinyume cha sheria na
kanuni za soka.

Hivo kwenye tukio la mechi ya jana Yanga wanahaki ya kulalamika,
kusikilizwa na kupewa alama zao tatu.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

72 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

HATIMAYE WENGER ANAIACHA ARSENAL: LAKINI NANI ANAFAA ZAIDI KUMRITHI?

Tanzania Sports

TULIMSUBIRI NEYMAR, AKAJA SALAH