Timu ya Kilimanjaro Stars ya Tanzania leo ilivuliwa rasmiĀ ubingwa Kombe la Afrika Mashariki na Kati Cecafa baada ya kutandikwa magoli 3-1 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Kilimanjaro Stars ilikubali kuvuliwa ubingwa katika mechi ya nusu fainali licha ya kujikakamua kwenye mchezo wa robo fainali ambapo iliifunga Malawi goli 1-0.
The Cranes yaĀ Uganda ndiyo iliyoidondosha chini Taifa Stars kwa na kufanye iungane naĀ Rwanda iliyoichabanga Sudan kwa magoli kama hayo na kutinga fainali pia.
Kwa matokeo hayo Tanzania nasubiri kuambulia ushindi wa tatu ama patupuĀ katika mchezo utakaofanyika Jumamosi kabla ya fainali yenyewe.
Mshindi wa kwanza atazawadiwa dola za Marekani 30,000 wakati wa pili atapata 20,000 na wa tatu dola 10,000.
Kipigo kwa Kilimanjaro Stars kiliendeleza mtindo wa timu za Tanzania kusindikiza michuano ya soka katika Bara la Afrika baada ya timu nyingine ya vijana chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes kuondolewa kwenye michuano ya vijana wa aina hiyo iliyoshirikisha nchi 10 chini ya Usimamizi wa Shirikisho la soka la nchi za Kusini mwa Afrika Cosafa.
Hata hivyo, Kilimanjaro Stars ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Mrisho Ngassa ,mshambuliaji mwenye kasiĀ aliyepachika goli baada ya kumnyangāanya mpiga kipa wa Uganda.
Lakini Uganda ilijibu pigo hilo dakika ya nane ya kipindi cha pili kupitia kwa Andrew Mwesigwa aliyefunga goli kwa kichwa.
Timu ya Tanzania ambayo iliingia kwenye robo fainali kwa ndondokelaĀ ilifanikiwa kumaliza dakika 90 kwa sare ya goliĀ 1-1.
NdiposaĀ muda wa nyongeza ulipoanza na katika dakika ya saba ya kipindi cha kwanza Emannuel Okwi wa Uganda alipachika goli lingine kwa kichwa na lingine lilipatikana kwa penati.
Okwi ambaye anachezea timu ya Soka ya SimbaĀ hakuona aibu kumfunga golikipa wa Simba Juma Kaseja ambaye kwa mechi hiyo alikuwa langoni akidakia Kilimanjaro Stars.
Kuhusu mechi ya kwanza, Rwanda ilifanikiwa kuitandika Sudan magoli 2- 1Ā katika mchezo mkali uliofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Itakumbukwa kwamba Rwanda iliingia robo fainali baada ya kuichapa Zanzibar magoli 2-1 piaĀ wakati nayo Sudan iliivurumisha Kenya magoli 2-0.