in , , ,

KAMATI YA RUFANI YA MAADILI YA TFF YAFANYA MAPITIO..

Kamati ya Rufani ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
imekutana jana (Oktoba 13 mwaka huu) kusikiliza maombi ya mapitio
(revision) na mwongozo ya uamuzi wa Kamati ya Maadili.

Sekretarieti ya TFF iliwasilisha maombi ya mapitio kwa Kamati hiyo ya juu
kabisa ya masuala ya maadili kutokana na ugumu wa utekelezaji wa uamuzi wa
Kamati ya Maadili juu ya mashauri nane yaliyowasilishwa mbele yake.

Kamati ya Rufani ya Maadili itaendelea na kikao chake kesho (Oktoba 15
mwaka huu), na baadaye itakutana na waandishi wa habari (saa 10 jioni) kwa
ajili ya kutangaza uamuzi wake juu ya mwongozo ulioombwa na Sekretarieti ya
TFF.

*KIONGOZI WA MWENGE AFUNGUA KITUO CHA IDYDCC*

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Juma Ali Amir amefungua kituo cha
kwanza cha Football for Hope kilicho mkoani Iringa kwa kuwataka wananchi
kukituia vizuri ili wanufaike na huruma za kijamii zinazotolewa na taasisi
ya IDYDC pamoja na kuendeleza mpira wa miguu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho jana (Oktoba 13 mwaka huu),
kiongozi huyo amesema taasisi ya IDYDC (Iringa Development of Youth,
Disabled and Child Care) wamefanya vizuri kuamua kutumia mpira wa miguu
kusaidia jamii kwa kuelimisha juu ya mambo mbalimbali kama ugonjwa wa
ukimwi, kusaidia walemavu, haki za watoto na afya ya jamii.

Naye Mwakilishi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA),
Patrick Onyango amesema amefurahishwa na kukamilika kwa kituo ambacho
kitasaidia jamii.

Amesema idadi kubwa ya watu waliofika kwenye uzinduzi huo inadhihirisha ni
kiasi gani kituo hicho kitakuwa na matokeo mazuri kwa jamii.

Onyango alisema hicho ni kituo cha 14 kukamilika kati ya 20 vinavyojengwa
barani Afrika ikiwa ni mpango wa FIFA kurudisha kwa jamii mafanikio
iliyopata kwenye fainali za kwanza za Kombe la Dunia barani Afrika.

Kituo hicho kina uwanja mdogo wa mita 20 kwa 40 uliowekwa nyasi bandia,
jengo lenye ukumbi wa mikutano kwa ajili ya semina, chumba cha kupimia
ukimwi, chumba cha ushauri nasaha, maktaba na ofisi.

Zaidi ya dola 270,000 za Marekani zimetumika kukamilisha ujenzi wa kituo
hicho kilicho eneo la Mtwivila, Iringa mjini.

*KESSY KUSIMAMIA MECHI YA KOMBE LA DUNIA*

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Mtanzania Lina Kessy
kuwa kamishna wa mechi ya Kombe la Dunia Kanda ya Afrika kwa wanawake chini
ya umri wa miaka 20 kati ya Botswana na Afrika Kusini.

Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza itachezwa nchini Botswana kati ya
Oktoba 25 na 27 mwaka huu. Waamuzi kutoka Zimbabwe ndiyo watakaochezesha
mechi hiyo namba tisa.

Waamuzi hao wataongozwa na Pamela Majo atakayepuliza filimbi wakati mwamuzi
msaidizi namba moja ni Rudo Nhananga, namba mbili ni Stellah Ruvinga na
mezani atakuwepo Tambudzi Tavengwa.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Ni Simba, Azam, Yanga

Halsey ‘awachana’ marefa