in

Julio, Mkwasa waondolewa Kili Stars

Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo linatarajia kutangaza kocha mwingine atakayeiongoza timu ya taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya wenzao wa Zanzibar Heroes itakayofanyika Januari Mosi kwenye Uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar.

Maamuzi ya kutangaza kocha mpya yametokana na makocha waliokuwa wakiiongoza wakati wa michuano iliyomalizika ya nchi za Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Chalenji) ambapo wenyeji Kili Stars walishinda mechi mbili tu kati ya sita walizocheza, Boniface Mkwasa na msaidizi wake Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ kuondolewa kwavile wanakabiliwa na majukumu mengine.
Hivi sasa, Mkwasa yuko ‘bize’ kuinoa timu ya taifa ya soka ya wanawake (Twiga Stars), ambayo inajiandaa kucheza dhidi ya Namibia katika mechi yao ya kuwania kufuzu fainali za Wanawake za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika jijini Harare, Zimbabwe.
Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, alithibitisha kuwa Mkwasa hataiongoza Kili Stars kwa sababu ya jukumu alilo nalo la kuiandaa Twiga na kwamba, wanalazimika kuteua kocha mwingine kwa vile Julio naye kwa sasa yuko nje ya nchi kwa shughuli nyingine za soka.
Osiah alisema kuwa jana, Idara ya Ufundi na Kurugenzi ya Mashindano ya TFF ilikuwa inamalizia kuteua kocha mwingine ambaye baada ya kutangazwa, (kocha huyo) ndiye atakayesema ni lini atataja kikosi chake na pia siku ya kuanza mazoezi ya timu hiyo.
“Kesho (leo) ndio tutamtangaza kocha atakayeiongoza timu hiyo,” alisema katibu Osiah.
Katibu huyo aliongeza kuwa wameshindwa kumpa timu hiyo kocha wa Taifa Stars, Jan Poulsen, kwa sababu hivi sasa yuko likizo, ingawa ameahidi kuwepo uwanjani siku hiyo kushuhudia mechi inayotarajiwa kuwa ya kuvutia baina ya ndugu hao, Kili Stars na Zanzibar Heroes.
Aliongeza kuwa tayari TFF imeshathibitisha kwa kwa Chama cha Soka cha Zanzibar (ZFA) kwamba itapeleka timu yake katika mechi hiyo maalumu ya ufunguzi wa mashindano ya kila mwaka ya Kombe la Mapinduzi.
Wakati huohuo, msemaji wa ZFA, Munir Zacharia, aliiambia NIPASHE jana kuwa maandalizi ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanaendelea vizuri na timu za kutoka Bara zitaanza kuwasili Zanzibar Desemba 31.
Simba ya jijini Dar es Salaam ndio mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi na katika michuano ya mwaka huu, iko Kundi A pamoja na timu za Miembeni, KMKM na Jamhuri ya Pemba wakati mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara,Yanga, wako Kundi B pamoja na Azam, Kikwajuni na Mafunzo.

Timu za Bara zinatarajia kutumia michuano hiyo pia kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara utakaoanza Januari 21 mwakani. Michuano hiyo pia inatoa nafasi ya kujiandaa kwa michuano ya kimataifa kwa wawakilishi wa Tanzania, klabu za Yanga na Simba

Enhanced by Zemanta

Report

Tottenham Hotspur

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Loading…

0

Mainland coach set to be named today

Year with practically nothing to show for