in , , , ,

GARY NEVILLE APIGWA CHINI VALENCIA

Valencia wamemtimua Gary Neville waliyemteua kuwa kocha wao mkuu miezi mitatu na wiki kadhaa zilizopita. Kibarua cha mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya England na Manchester United kimeota nyasi kufuatia mfululizo wa matokeo mabaya.

Chini ya kocha huyo Valencia wameshinda michezo mitatu pekee kati ya michezo 16 ya Ligi Kuu ya Hispania huku wakiibuka na ushindi mara 10 kwenye michezo 28 ya mashindano yote.

Mbaya zaidi chini ya kocha huyo Valencia wameruhusu bao ama mabao kwenye kila mchezo kati ya michezo yote 16 ya La Liga. Wameruhusu jumla ya mabao 25 kwenye idadi hiyo ya michezo ya La Liga.

Wakati Neville alipokabidhiwa mikoba timu ilikuwa kwenye nafasi ya 9 na sasa inashikilia nafasi ya 14 ikiwa na alama 6 pekee zinazoitenganisha na ukanda wa kushuka daraja. Pengine hofu ya kushuka daraja ndiyo iliyowafanya Valencia kuamua kuachana na Neville.

Watendaji wa klabu hiyo ya Hispania wameonesha uvumilivu wa kutosha kwa kocha huyo lakini sasa uvumilivu wao umefikia kikomo kufuatia kipigo cha 2-0 kutoka kwa Celta Vigo siku chache kabla ya mapumziko ya kupisha michezo ya kimataifa.

Kipigo hicho kilikuwa cha tatu mfululizo kwa timu hiyo kwenye La Liga ikiwa imebaki michezo nane pekee kuelekea ukingoni mwa msimu.

Pengine matokeo ya Valencia kwenye michezo ya Kombe la Mfalme na Ligi ya Europa ambapo wameshinda michezo 7 kati ya 12 ndiyo yaliyowafanya wamiliki wa timu wampe nafasi ya kujaribu kurekebisha makosa yake.

Ilitarajiwa kuwa kocha huyo angetimuliwa Februari mwaka huu baada ya kupokea kipigo cha 7-0 dhidi ya Barcelona kwenye mchezo wa Kombe la Mfalme. Hicho kilikuwa kipigo kizito zaidi kwa Valencia kwenye mchezo wa kombe ndani ya Hispania tangu 1928.

Pako Ayestaran ndiye atakayeiongoza timu katika kipindi cha msimu kilichobakia. Kocha huyo msaidizi wa zamani wa Liverpool atakuwa na kibarua chake cha kwanza Jumamosi dhidi ya Las Palmas walio nafasi moja chini ya Valencia kwenye msimamo wa La Liga.

Ayestaran anakutana na kibarua cha kuhakikisha timu hiyo haishuki daraja. Sevilla, Barcelona, Villareal na Real Madrid ni miongoni mwa timu atakazokabiliana nazo kwenye michezo 8 ya La Liga iliyosalia.

Kuhusu kubaki na Phil Neville ambaye ni ndugu wa Gary kama sehemu ya benchi lao wakufunzi, Valencia bado hawajaweka wazi. Hata hivyo inaaminiwa kuwa Phil anaendelea kubaki kama kocha msaidizi.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote
Tanzania Sports

Tuliyojifunza kwenye mechi za kirafiki kuelekea Euro

Tanzania Sports

AZAM, YANGA ZAFUZU NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO