in

FAINALI EUROPA

Unai Emery

Ole, ubora na udhaifu wa Man United

Rafiki yangu mmoja kutoka Afrika kusini ambaye ni shabiki wa Manchester United alinitumia picha ya kocha wa zamani wa tiu hiyo Sir Alex Ferguson akiwa ameketi meza ya chakula na wachezaji Nemanja Matic na Edinson Cavani huku wakiwa wamejawa na tabasamu.

Shabiki huyo alituma picha hiyo kwangu kabla ya mchezo wa fainali ya Kombe la Europa League dhidi ya Villareal ya Hispania. Kila shabiki ana matumaini makubwa kwa timu yake. hivi ndivyo alivyofanya rafiki yangu huyo, na ikabidi nimfurahie kujiamini kwake.

Mashabiki wengi wapo hivyo mbele ya wenzao hata kama watakuwa na mashabiki juu ya uwezo wa ti u yao kushinda mchezo mbali ya kunyakua taji lililope mbele yao. Man United wana kibarua kigumu mbele yao na si rahisi kama wanavyodhani. Mwisho wa mchezo Villareal ilishinda taji la Europa kwa ushindi wa matuta 11-10 baada ya kumaliza dakika 120 wakiwa sare 1-1

KIVULI CHA FERGUSON

Tabasamu la Ferguson katika picha aliyotuma rafiki yangu huyo lilinikumbusha kuwa kwa sasa afya yake ni imara na inakwenda vema. Lakini uwepo wake mbele ya wachezaji hao ulinikumbusha mambo kadhaa nyuma.

Alikuwa Ferguson mtemi, mkono wa chuma,shupavu,jabali na kiongozi aliyeshika kila kona ya damu za Man United kuanzia miili ya mashabiki na mazingira yake kwa ujumla.

Ferguson kuonekana kwenye kambi ya wachezaji wa Man  united kunaniambia kuwa yeye ndiye mtu aliye karibu zaidi na benchi la ufundi. Wakati akitangaza kuwa angeachia ngazi mwaka 2002, ghafla alibadili mawazo na kuednelea kuinoa Man United.

Tanzania Sports
Unai Emery

Ulikuwa uamuzi mgumu kuachana na Man United aliyodumu nayo tangu mwaka 1986. Lakini uamuzi wake wa pili mwaka 2013 ulikuwa wa moja kwa moja kuwa anang’atuka kuinoa timu hiyo.

Hata hivyo bado kivuli cha Ferguson kimeendelea kuwatesa makocha wengi waliokabidhiwa timu hiyo. Kuanzia David Moyes aliyetokla Everton na kutarajiwa kufanya makubwa kwenye timu yenye bajeti kubwa, lakinia akashindwa. Akaja jina kubwa Luis van Gaal, mambo yakawa magumu zaidi.

Amepita Jose Mourinho na Ryan Giss bado Man United haikurudi kwenye uwezo ule aliokuwa nao Ferguson. Man United ya kutwaa makombe, ikitetemesha wapinzani wake EPL si hii ya sasa.

Kwenye Ligi ya Mabingwa ndiko palikuwa mahali pake kila msimu, lakini Man United bila Ferguson inabanduliwa huko Europa League. Kwamba Man United imekuwa ya kucheza Europa siku hizi na imewahi kutwaa taji hilo chini ya Mourinho.

Man United bila Ferguson haiogopwi. Uwanja wake wa nyumbani inazabwa mara nyingi, sina sababu ya kurudia takwimu zake. huo ni ujumbe Man United haijapata kocha sahihi wa kuifikisha kwenye hadhi aliyoweka Alex Ferguson.

Hata uwepo wake kambini maana yake ni kuongeza chachu na mawaidha kwa wachezaji lakini bado haisadii na Ferguson hana uwezo wa kurejea kwenye kiti hicho tena kwani anachunga afya yake. siku kivuli cha Ferguson kikiondoka ndipo Man United itaweza kusonga mbele. Hali hiyo inawakumba pia wenzao Arsenal ambao wanahangaika angalau kufikia robo ya ufanisi wa kocha wao wa zamani Arsene Wenger. Kivuli cha Wenger bado kinawatafuna, nao wamebadilisha makocha.

UBORA NA UDHAIFU

Ukiangalia wachezaji wa sasa wa Man United ni kizazi kingine sio kile cha nguvu na mapafu ya mbwa kama ilivyoelekea. Wachezaji waliopo sasa ni wale wa kizazi kipya na wamejitajidi kusajili kwa kiasi fulani.

Tatizo lililopo ni kukosa wachezaji wenye uzoefu wa mashindano makubwa na walioiva kwa kupambana msimu mzima. Kwenye mchezo wa fainali ya Europa ukitazama kikosi chao utaona wachezaji wasio na uzoefu ni Greenwood,Rashford,Wan Bissaka,McTmonay,James,Tuanzebe, ndio wanakuwa tegemeo. Wachezaji wenye uzoefu Cavani,Pogba,De Gea,Bailly walikosa huduma ya wenzao wenye kaliba yao.

Namna wanavyocheza, wanamiliki mpira vizuri lakini hawana safu ya ushambuliaji ya kutisha wala viungo wabunifu kama zilivyo timu zingine. Man United kufika fainali ni jambo la kuheshimiwa, lakini kushinda mchezo wa fainali unahitajika kuwa na wachezaji wanaojua kufanya kazi ngumu kuwa rahisi.

Wachezaji ambao wanatengeneza muunganiko na watu kama Cavani, yaani angezu gukwa na majembe ya uhakika upande wa kulia,kushoto na nyuma yake. ninaamini kwa hali waliyonayo walihitaji kiungo mbinifu na McTominay angewekwa pembeni kumpisha Juan Mata kwenye kikosi cha kwanza.

Mata ana uwezo mkubwa wa kupiga pasi za mwisho kulio kinda McTominay. Vinginevyo, kama Ole Gunnar Solskjaer atavumiliwa basi wanakiwa kuwa watulivu kama wenzao Arsenal walivyojenga timu ya vijana na ikapoteza fainali ya kombe la Carling kwa makosa ya golikipa na mabeki wake. Chipukizi anafanya makosa siku ya fainali inabidi umeze hivyo hivyo hata kama ni ya moto; wavumiliwe hadi wakikomaa.

Lakini kwa kikosi chao cha sasa licha ya vipaji walivyo nayo bado haviwapi nafasi ya kutoa kitu cha ziada kwenye mashindano makubwa. Ndio maana unashangaa mchezo wa fainali umemalizika nahodha Bruno Fernades analia, badala ya kuvaa uhusika wa uongozi kuwapa pole wenzake, kazi iliuyofanywa na Edinson Cavani.

Pengine Man United wanajaribu kutengeneza timu kwa falsafa ya Ferguson aliyoibua wachezaji maarufu kama ‘Class of 1992 Paul Scholes, Nick Butt,David Beckham,Gary Nveille,Phil Nveille, na Ryan Giggs ndiyo inakwenda kuwabebea akina McTominay, Greenwood, Rashford, Tuanzebe, James. Huu ndio udhaifu na ubora kwa wakati mmoja kwa sababu viwango vya vijana hawa si vya kushindana na majabali wa soka.

OLE ‘ATAMTEMA’ FERGUSON?

Kimsingi kivuli cha Ferguson kinaonekana kupitia kubaki kwa kocha wa Man United. Ni wazi uongozi unataka kusimamia mpango maalumu wa kuirudishia makali timu hiyo kupitia vipaji vya ‘Old Trafrord’. Lakini hasara mojawapo ni kushindwa kutwaa taji mbele ya Villareal ambayo haikuwa kigogo kwenye mashindano hayo.

Lakini je, Ole Gunnar Solskjaer licha ya kuwa mchezaji mahiri enzi zake hapo hapo Old Traford, anafaa kuendelea kuinoa Man United? Je mbinu za Ole zinaridhisha mbele ya magwiji wa soka?

Ikiwa Man United leo imekuwa ikshindwa hata kutwaa taji la Europa, ni lini watakuwa na uwezo wa kupigania Ligi ya Mabingwa kama enzi za Ferguson?

Je wataweza kurudisha enzi hizo chini ya Ferguson? Kwa hali waliyonayo Man United kwa sasa ni kama vile benchi la ufundi limeshindwa kuvutia wachezaji wakali.

Benchi lenye Ole Gunna Solskjaer na Michael Carrick litaweza kufurukuta kwenye Ligi ya Mabingwa kama zama za Ferguson? Kwa mbinu zipi? Maswali ni mengi, Ole atawekwwa alama ya kuuliza kwa nia ya kutiliwa shaka mbinu za kuipaisha Man United katika ushindani waliokuwa nao awali.

Report

Written by Mark Mpangala

*Markus Mpangala ni Mhariri, Mwandishi wa Makala Maalumu, Mwanahabari,Mwanablogu,Mwanafasihi na Mwanasafu, ambapo kwa kipindi cha miaka 12 amefanya kazi katika vyombo vya habari mbalimbali vikubwa na vidogo nchini Tanzania katika Michezo, Siasa, Elimu na utalii. Pia ni mchambuzi mchangiaji wa masuala ya siasa na utawala bora katika idhaa ya Kiswahili ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC SWAHILI). Ni mhariri na mhamasishaji wa usomaji wa vitabu*

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Manchester City vs Chelsea Champions League final

Fainali ya UEFA bila washambuliaji

Manchester City and Chelsea meet in the Champions League final

Fahamu mambo adimu kuelekea fainali UEFA leo