in

Fahamu mambo muhimu mchezo wa Arsenal vs Chelsea

ARSENAL imemaliza michezo miwili ikiwa haijapata alama zozote hivyo kubakiwa na mechi 36 za Ligi Kuu England. Chelsea wamepata alama 6 baada ya kushinda micheo yao miwili ya awali wakiwa wamebakiwa na mechi 36 mkononi. Arsenal walikawaribisha mabingwa wa Ulaya, Chelsea katika dimba lao, huku wakiwa na maumivu ya kufungwa na wageni wa Ligi hiyo Brendford wiki moja iliyopita.

TANZANIASPORTS imefanya tathmini ya mchezo huo ambao ulikuwa wa pili kukutanisha vigogo wa soka EPL baada ya Tottenham Hotspurs kumenyana na mabingwa watetezi Manchester City katika mchezo wa ufunguzi. Yafuatayo ni mambo muhimu katika mchezo wa Arsenal na Chelsea.

KAZI CHAFU

Katika safu ya ulinzi ya Arsenal kwenye mchezo wao dhidi ya Chelsea kulikuwa na mabeki wawili Holding na Pablo Mari. Lakini mabeki hao hawakuonesha wanajua kazi chafu ya mabeki wa kati. Hii ni dhana ambayo inatakiwa kuwa na beki ambaye anakuwa anachea mchezo wa nguvu na ubabe muda wote wa dakika 90 lakini hauna madhara kwa timu yake.

Katika ,mabeki wanaojua kazi chafu kwa upande wa Chelsea alikuwa Antonio Rudiger. Muda wote wa mchezo alikuwa akiwachezea ubabe washambuliaji wa Arsenal kuanzia Martinelli,Bukayo Saka,Bolagun na Aubameyang.

Kwa Chelsea wana mabeki wa aina hiyo Kurt Zouma na Rudiger. Arsenal wanaonekana kucheza kiheshimiwa sana yaani ile hali ya timu kucheza kwa uangalifu kiasi kwamba inaonesha kana kwamba wapo kwenye mazoezi ya kawaida na hawakuweza kuonesha umahiri katika kazi chafu mbele ya wachezaji wa Chelsea.

BURUDANI BILA MIPANGO

Burudani wanayotoa Arsenal ni nzuri, lakini haikuonesha kuwa ina mipango yoyote hatarishi mbele ya safu ya ulinzi ya Chelsea. Umiliki wao wa mpira ni kiburudiosho tosha kwani kuna wakati waliongoza kwa asilimia 85 dhidi ya 13 za Chelsea. Hata hivyo burudani hiyo ilikosa mipango sahihi na hapakuw ana silaha ya kuimaliza Chelsea.

Mashambulizi mengi yalikwenda lakini hayakuwa na madhara na mpango wa kupata mabao haukuwa wazi kwa Arsenal. Ukizingumzia vipaji basi Arsenal walikuwa na vipaji murua kabisa. lakini tatizo lilikuwa katika mipango,mwelekeo sahihi au mbinu mahususi za kuibuka na ushindi, hakika hazikuonekana.

STAMINA

Tanzania Sports
Lukaku akiwakimbiza mchakamchaka

Wachezaji wa Chelsea walikuwa wanaongoza kwa matumizi ya nguvu, kiasi kwamba walikuwa wanawaathiri Arenal wakati wakikabiliana kimwili. Stamina hiyo pia ilikuwa tatizo kwa Arsenal kwa sababu walijikuta wakipoteza mipira mingi kirahisi mno mbele ya wapinzani wao. Ni jambo ambalo linaleta wasiwasi kuona wachezaji wa Arsenal kukosa stamina ya mchezo.

Utimamu wao wa nguvu haukuonekana katika mchezo dhidi ya Chelsea. Kuna kazi ya kufanya kwa walimu wa viungo kuwaongezea “chakula’ (nguvu) wachezaji wao ili kusaidia maarifa katika utendaji wao wanapokabiliana na timu yenye matumizi makubwa ya nguvu.

Jambo hilo tumeliona likilalamikiwa na kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ambaye alisema wachezaji wa Burnley wanatumia mabavu miili yao zaidi hali iliyowaumiza wachezaji wake. Hakika Burnley walionekana wamepewa mazoezzi ya nguvu ya utimamu wa miili yao, jambo ambalo Arsenal watapata shida kucheza na timu kama hiyo.

UTATANISHI WA KOCHA

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta ni lazima abebeshwe lawama kufungwa kwao na Chelsea. Sababu dakika 45 za kipindi cha kwanza ndizo zlizoiangamiza timu yake, ilikosa mpango sahihi wa kushambuliaji na hawakuwa tishio mbele ya Chelsea.

Upangwaji wa safu ya ushambuliaji ulionesha utatanishi zaidi. kumpanga Martinelli kuwa mshambuliaji kamili lilikuwa jambo bora kujaribu mbinu mbadala baada ya kuwaweka nje Pierre Emerik Aubameyang na Lacazette. Lakini Mikel Arteta hakuwa sahihi kumweka benchi nahodha wake Aubameyang kwa sababu yeye ndiye angekuwa silaha ya kushambuliaji akiwa pacha wa Martinelli.

Kuwapanga Smith Rowe na Bukayo Saka kulionesha wazi wanatabirika na hawakuwa na uwezo wa kuisukuma safu ya ulinzi ya Chelsea. Bukayo upande wa kushoto hakuwa mahiri wala hakuwa na uamuzi wa haraka na ubunifu. Smith Rowe alikosa umakini kiasi kwamba timu nzima ikawa haipati bao. Umakini wao katika eneo la hatari ulikuwa hafifu mno.

KIUNGO DHAIFU

Tanzania Sports
Arteta

Eneo la kiungo cha Arsenal ni dhaifu, lakini Chelsea wanafichwa na uwezo wao kucheza vizuri maeneo ya pembeni. Chelsea walituia zaidi upande wa kulia walikompanga James, na kushoto ambako alikuwepo Mount. Wawili hawa walikuwa wanacheza kwa kasi na ndiyo kiini cha kuirudisha nyuma Arsenal.

Pengine Ben Chilwell ana kasi na uwezo mzuri wa kukokota mpira na kufanya maamuzi ya haraka kuliko Marcos Alonso, lakini kushindwa kwa Arsenal kudhibiti mawinga wa Chelsea kulisababisha timu iyumbe katikati ya dimba. Huduma hafifu ya Rowe,Xhaka na Sambi kilikuwa chanzo cha wao kupoteza mchezo huo.  Suluhisho la eneo hilo lilikuwa ni kupanga viungo watano katika mfumo wa 4-5-1 ambao wangedhibiti kasi ya Chelsea kupitia pembeni.

Kwa kujua eneo la kiungo la Arsenal lina wachezaji wapya ambao bado hawana moto, kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel alimweka benchi Ng’olo Kante hali ambayo inaonesha alitaka kucheza mchezo wa wazi zaidi. na katika uwazi huo huo Arsenal walishindwa kupenya eneo la Jorginho.

WATOTO WENGI

Kikosi cha Arsenal kiliundwa na watoto wengi mno. Mabaidliko yao yalionesha mtu mkubwa ni Aubameyang, lakini wengine walioingia ni watoto. Wastani wa umri wa kikosi cha Arsenal ni chini ya miaka 25. Unaweza kurudisha kumbukumbu ya mchezo husika kisha gawanya na umri wa Chelsea. Wengi wa wachezaji wa Chelsea wana uzoefu na walitumia mwanya huo kuwahenyesha Arsenal. Watoto wa Arteta walijikuta wakipoteza mipira kirahisi mno kiasi kwamba timu ikawa inakosa mpango maalumu wa kuiteketeza Chelsea.

KIONGOZI NANI?

Arsenal ineonekana kukosa kiongozi kwenye safu ya ulinzi. Mabeki waliocheza dhidi ya Chelsea hawaridhishi. Kama unamweka benchi Aubameyang maana yake unapatakiwa kuwa na kiongozi mwenye uzoefu uwanjani.

Lakini Xhaka hakuweza kuwa nao uongozi hata eneo la kiungo hivyo kuifanya timu iwe inatembea badala ya kukimbia kuelekea lango la adui. Arteta alikosa kiongozi thabiti wa mpango wake wa mchezo kutafuta ushindi, na hata kipindi cha pili kilipofika dakika 75 ilionesha wazi bado hapakuwa na mtu wa kuiongoza Arsenal ndani ya dimba.

MPANGO WA PILI WENYE MASHAKA

Chelsea wamempata mshambuliaji waliyemtaka, Romelu Lukaku. Katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Arsenal alipachika bao. Ndiye alikuwa mshambuliaji anayewatesa mno mabeki wa Arsenal kwa kutumia mwili wake, nguvu na maarifa. Lakini ukitazama mpango wa pili unamwona Timo Werner katika safu ya ushambuliaji. Inatia mashaka, kwamba katika mechi 38 za EPL ni nyingi na kati ya hizo Lukaku anaweza kupotea pia.

Sababu matumizi yake ya sasa yameanza kuonekana kwahiyo makocha watakuwa na kazi ya kumsoma Tuchel na Lukaku wanataka kufanya nini na namna ya kuwazuia. Sasa katika mpango wa pili maana yake atakuwepo Timo Werner, na labda Pulisic, hilo lina maana ukata wa mabao utaielemea Chelsea ikiwa mpango wa kwanza (Lukaku) utafeli. Hapo ndipo yaliyopo mashaka, msimu atamalizaje?

Hali kadhalika, Arsenal hawaonekani kuwa na mpango wa pili, kwa sababu hata wa kwanza bado hauna maarifa hivyo si rahisi kuuita ni mpango wa kwanza. Mikel Arteta atalazimika kuketi chini na kukubali mpango wake dhidi ya Chelsea ulikuwa hafifu na anatakiwa kufumba macho kumpa majukumu Aubameyang kuongoza safu ya ushambuliaji. Kinyume cha hapo labda aingie sokoni ndani ya siku 7 anunue mshambuliaji mpya wa kuongeza nguvu.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Liverpool FC

Jurgen Klopp ana kibarua kigumu

Luis Miquissone

Mambo usiyoyajua kuhusu usajili wa Miquissone