in , , , ,

De Gea pasua kichwa

*Van Gaal: Sijui kwa nini hataki
*Livermore abambwa na cocaine

Manchester United wanajiandaa na maisha bila kipa wao namba moja, David De Gea ambaye hadi sasa hajakubali kusaini mkataba mpya aliopewa.

Kocha Louis van Gaal amesema hajui kwa nini De Gea hataki kusaini mkataba mpya hata baada ya kupewa ofa ya mshahara wa pauni 150,000 kwa wiki.

Van Gaal amesema klabu imeshaandaa orodha ya makipa watakaochukua nafasi yake iwapo ataondoka Old Trafford.

Mkataba wa De Gea, 24, unamalizika kiangazi cha mwaka kesho na anadaiwa kutaka kujiunga na Real Madrid.

“Tunayo orodha ya magolikipa wanaoweza kuchukua nafasi yake kwa sababu lazima tujipange. Tunataka abaki na asaini mkataba mpya. Kuna pande tatu lakini mwenye nguvu zaidi ni mchezaji mwenyewe.

“Kusaini kwake hakutegemei Manchester United wala mimi, kwa sababu tunataka asaini lakini uamuzi ni wake, sasa sijui kwa nini hajaamua,” anasema Van Gaal.

Majadiliano na mzaliwa huyo wa Madrid aliejiunga na Man U 2011 akitoka Atletico Madrid yalianza mapema msimu huu, ambapo Van Gaal anadai wamempa ahadi ya ‘fedha nyingi’ ili abaki.

Van Gaal alitumia zaidi ya pauni milioni 150 kununua wachezaji wapya saba mwanzoni mwa msimu huu.

Makipa wanaodaiwa kwua kwenye orodha ya Van Gaal ni pamoja na Hugo Lloris wa Tottenham Hotspur na Samir Handanovic wa Internazionale.

Kadhalika sasa wanataka kumchukua Petr Cech wa Chelsea ambaye ameshapewa ruhusa ya kuzungumza na klabu zinazomtaka, lakini kocha Jose Mourinho angependa kumuuza nje ya England.

Arsenal wanamtaka kipa huyo sambamba na Paris Saint-Germain (PSG) na Besiktas ambao wanadaiwa kuanza mazungumzo.

De Gea alipoulizwa iwapo angeweka tarehe ya mwisho ya kuamua hatima ya De Gea alisema:

“Unapokuwa na tume nzuri ya wang’amuzi kama yetu basi tunakuwa tayari tumeshajua nani atakuwa kipa wetu ajaye. Tuna orodha ya kila nafasi. Sijui De Gea atachukua uamuzi gani.”
Real Madrid katika mipango ya kumsajili De Gea wamemwahidi


LIVERMORE WA HULL NA COCAINE

Kiungo wa Hull, Jake Livermore (kushoto) amedaiwa kubwia dawa za kulevya aina ya cocaine na klabu yake pamoja na Chama cha Soka (FA)
Kiungo wa Hull, Jake Livermore (kushoto) amedaiwa kubwia dawa za kulevya aina ya cocaine na klabu yake pamoja na Chama cha Soka (FA)

Kiungo wa Hull, Jake Livermore amedaiwa kubwia dawa za kulevya aina ya cocaine na klabu yake pamoja na Chama cha Soka (FA) wamemsimamisha.

Livermore aliyejiunga na Hull Juni mwaka jana kutoka Spurs kwa ada ya pauni milioni nane sasa ataendelea kuchunguzwa ma FA wakati Hull wakifikiria hatua za kinidhamu za kumchukulia.

Livermore amepata kuchezea Timu ya Taifa ya England mechi moja, ikiwa ni ile ya kirafiki dhidi ya Italia Agosti 2012 na ameichezea Hull mechi 39.

Wachezaji wanaopimwa na kukutwa wametumia dawa za kulevya zisizoruhusiwa, tofauti na zile za kuongeza nguvu, wanaweza kufungia hadi miaka miwili kucheza soka, kwa mujibu wa kanuni za FA.

Kabla ya kusajiliwa moja kwa moja Hull, Livermore alikuwa kwa mkopo katika klabu hiyo, na nyingine za MK Dons, Derby, Peterborough, Ipswich na Leeds.

Amesaini mkataba wa miaka mitatu na Hull, klabu wakiwa na uwezekano wa kuongeza miezi 12. Hili ni pigo kwa klabu ndogo waliotumia ada kubwa kumnunua, na ambao wanashika nafasi ya 18 kwenye msimamo wa Ligi Kuu, wakielekea kushuka daraja.

Ilikuwa Jumamosi hii Livermore aingie dimbani katika klabu yake ya zamani, Spurs, wanakocheza kutafuta kujinasua kushuka daraja na watamaliza mechi zao kwa kukipiga na Manchester United Mei 24.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Waziri wa michezo Ivory Coast atimuliwa

La Liga ruksa kuendelea