in , ,

Dakika za mwisho za usajili zilivyotikisa

Dirisha la Usajili katika Ligi Kuu ya England (EPL) limefungwa baada ya kuwa wazi tangu Julai mosi.
Klabu za Tottenham Hotspur na Manchester City zimeonekana kuchangamkia zaidi usajili dakika za mwisho.
Klabu nyingi zilitumia mbinu tofauti, ziwe za ushawishi, fedha au ujanja wa kutazama upepo hadi  kupata wachezaji zilizoona watazifaa.
Usajili wa majira ya kiangazi umeshuhudia Charlie Adam wa Liverpool akienda Stoke City, huku Patrick Agyemang wa QPR akitimkia Stevenage kama mchezaji huru.
Joey Barton aliyekuwa na matata Queen Park Rangers (QPR) ameondoka kwa mkopo kujiunga Marseille ya Ufaransa.
Yossi Benayoun wa Chelsea aliyekuwa Arsenal kwa mkopo msimu uliopita kaenda West Ham United kwa mkopo tena.
Katika utaratibu wa kupunguza mizigo, Arsenal imemtoa Nicklas Bendtner kwa Juventus kwa mkopo.
Aston Villa imempata Christian Benteke wa Genk wakati Dimitar Berbatov wa Manchester United aliyetikisa kwa dau kubwa la usajili alipoingia Manchester ametua Fulham siku ya mwisho bila kutarajiwa.
Dirisha limeshuhudia Nigel de Jong wa Manchester City akihamia AC Milan ya Italia wakati nyota Clint Dempsey wa Fulham aliyetaka kwenda Liverpool akitua Tottenham Hotspur.
Kocha Andre Villas-Boas wa Hotspur amemwachia Giovani dos Santos kwenda Real Mallorca ya Hispania.
Michael Essien wa Chelsea aliyekuwa amekosa namba kikosi cha kwanza amehamia Real Madrid.
Manchester City imemnasa Javi Garcia wa Benfica kwa donge nono.
Klabu inayoibukia kuwa tishio ya Swansea nayo haikuwa nyuma, kwani imemchukua Pablo Hernandez wa Valencia ya Hispania.
Chelsea ya Roberto di Matteo nayo imepunguza gharama kwa kumtoa Gael Kakuta kwa mkopo kwenda Vitesse Arnhem.
Tottenmah imejiimarisha zaidi kwa kuchukua golikipa mahiri – Hugo Lloris wa Lyon ambaye ni namba moja na nahodha wa timu ya taifa ya Ufaransa.
Manchester City waliokuwa kimya siku za mwanzo za usajili wamefanikiwa katika dakika za mwisho kumnasa Mbrazili Maicon kutoka Internazionale.
Roberto Mancini pia amemnasa Matija Nastasic kutoka Fiorentina kuwaongezea nguvu matajiri hao wa Manchester.
QPR iliyoanza ligi vibaya nayo imejitutumia si haba, kwa kumpata Stephane Mbia kutoka Marseille ya Ufaransa.
Stoke City inayoendelea kujipambanua kama timu ngumu uwanjani, imempata Steven Nzonzi wa Blackburn, wakati wakati Bryan Oviedo wa Copenhagen amekwenda Everton.
Arsenal tena imemtoa Park Chu-Young kwa mkopo kwenda Celta Vigo, huku Goran Popov wa Dynamo Kiev akitua kwa wagumu wengine wa West Brom.
Wageni katika EPL – Southampton nao walijikusanya na kwenda hadi Italia walikompata Gaston Ramirez wa Bologna wakati Kieran Richardson katoka Sunderland kwenda Fulham.
Danny Rose wa Tottenham amekwenda Sunderland kwa mkopo, huku Stefan Savic wa Manchester City akienda Fiorentina.
Swansea imekubali kumuuza mchezaji wake mahiri Scott Sinclair kwa Manchester City, huku nyota wa Tottenham, Rafael van der Vaart akienda Hamburg ya Ujerumani.
Baada ya kukamilika kwa kipindi cha usajili, kuanzia wikiendi ijayo ni wakati wa kushuhudia timu zilizokamilika zimavyojituma uwanjani kuwania pointi muhimu.
Dirisha limefungwa wakati EPL ikiingia kwenye mzunguko wa tatu, japokuwa klabu zitaweza kuwatumia vyema wachezaji waliochelewa kuanzia mzunguko wa nne na mizunguko inayofuata.
Kilichobaki sasa ni kushuhudia jinsi makocha watakavyowapanga wachezaji wa zamani na wapya waliowaongeza, na wachezaji wenyewe watakavyojituma.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Timu zaanza kujichuja msimamo EPL

SPORTS ENHANCES THE SPIRIT AND ECONOMICS