in

Dakika 33 za dhahabu za Paul Pogba

Manchester United’s Paul Pogba

Hapana shaka mashabiki wa Manchester United walikuwa wamemkumbuka Paul Pogba. Majeraha yalimweka mbali na uwanja. Uwanja ambao huwakutanisha yeye na mashabiki wa Manchester United.

Mashabiki ambao huwajawahi kunyamaza hata kipindi cha njaa. Kwao wao wanaamini timu yao ni bora na yenye mafanikio makubwa kuliko timu yoyote. Huwezi kuwakataza kwenye huo mtazamo wao.

Mtazamo ambao umebaki kwa kipindi kirefu. Mtazamo ambao unaenda mpaka kwa wachezaji wao. Mashabiki wa Manchester United wanaamini wao wana wachezaji bora na imara kuliko timu yoyote.

Ndivo walivyozaliwa huwezi kuwabadilisha. Kujikweza ndiyo desturi yao na wanajivunia sana kwenye hii desturi yao. Wanaweza kumweka juu Bruno Fernandez mbele ya Kelvin De Bruyne.

Kwao wao Marcus Rashford ni bora zaidi ya Mbappe. Huwezi kuwabadilisha kwenye hili. Tuachane na kujivuna kwao, turudi hapa, Wakati ambao Paul Pogba yuko kwenye majeraha kulikuwa na maneno mengi sana kumhusu yeye kutoka kwenye midomo ya mashabiki wa Manchester United.

Kuna mashabiki wa Manchester United ambao waliamini kabisa Paul Pogba ana kiburi, hataki kurudi uwanjani na hataki kabisa kuwa mmoja wa wachezaji wa Manchester United baada ya tetesi nyingi kuzagaa kuwa anaenda Real Madrid wakati mwingine kulikuwa na tetesi kuwa anarudi Juventus.

Hawa mashabiki walikuwa na chuki kidogo kuhusu Paul Pogba. Mashabiki ambao jana walikuwa wanamsubiria kwa hamu sana Paul Pogba akanyage nyasi za uwanja wa Tottenham Hotspurs kwa ajili ya mechi ya ligi kuu ya England.

Miguu yake ilibahatika kugusa mpira kwa muda wa dakika 33 tu. Dakika ambazo zilikuwa za dhahabu, dakika ambazo zilimwezesha Paul Pogba aisaidie timu yake kusawazisha goli na timu yake kupata alama moja.

Alama ambayo imewaweka katika nafasi ya tano, nafasi ambayo wako nyuma ya alama mbili na timu inayoshika nafasi ya nne (Chelsea) pamoja na kwamba Manchester United wako mbele kwa mchezo mmoja lakini wanazidi kuwa na matumaini makubwa ya kufuzu ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Mpaka sasa hivi Manchester United hawajafungwa katika michezo 12 iliyopita. Na katika michezo mitatu iliyopita wameruhusu magoli matatu tu, kitu ambacho kinaonesha kuwa kwa sasa timu inajilinda vyema.

Pamoja na kwamba timu inajilinda vyema De Gea anaonekana kama mtu ambaye anaiangusha safu yake ya ulinzi kwa kufanya makosa mengi ambayo yanaigharimu timu yake. Jana ilikuwa mechi ya Paul Pogba kuwasema watesi wake na ilikuwa mechi ya David De Gea kujiharibia.

Report

Written by Martin

Martin Kiyumbi ni mchambuzi wa habari za michezo na mbunifu wa maudhui.

Martin Kiyumbi amewahi kufanya kazi za uchambuzi kwenye vituo mbalimbali vya habari kama Tanzaniasports (tovuti ya habari za michezo ), Jembe FM , Radio Free Africa na TVE.
Martin Kiyumbi anapatikana kwenye e-mail ya [email protected]

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0
Mchezaji wa Azam FC

Yanga, Azam FC utamu wake uko hapa

Tanzania Sports

Simba SC Kuukaribia Ubingwa