in , , ,

Benitez: Chelsea msihofu, naondoka

*Awatolea uvivu mashabiki wanaompinga

*Aivaa bodi kwa kumpa ukocha wa muda

*Agombana na Terry, baada ya kichapo cha Man City

 

Kocha wa muda wa Chelsea ameonesha hasira kali, akawabwatukia mashabiki wanaompinga, akisema bado kidogo ataondoka.

Benitez aliyechukua nafasi hiyo kutoka kwa kipenzi cha mashabiki, Roberto Di Matteo amekuwa akisema atawavuta mashabiki, lakini Jumatano hii ameonekana kuishiwa uvumilivu.

Alisema isiwe tabu kuwapo kwake Stamford Bridge, maana anafundisha kwa mkataba hadi mwisho wa msimu tu, hivyo bora mashabiki wakaiunga mkono klabu yao ifanikiwe.

Mhispania huyo aliyepata umaarufu kwa kuzoa makombe katika nchi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kombe la dunia la klabu, anachukiwa na mashabiki kwa sababu ya uhasama uliojengwa alipowafundisha Liverpool kwa mafanikio makubwa.

ba

Benitez alisema mabango yanayoendelea kuoneshwa kama vile ‘Rafa Benitez Out!’ au kumpigia kelele hakutamyumbisha, kwani anaijua kazi iliyompeleka hapo na ataikamilisha, awaache baada ya Mei mwaka huu.

Aliwananga pia viongozi katika bodi ya klabu hiyo kwa kubandika neno ‘kocha wa muda’ katika cheo chake, akisema labda walilenga kunawa mikono kwa wadau wengine, kuonesha kwamba kwa vile alitoka Liverpool hatamudu na hatakaa sana.

Benitez ambaye kwa kawaida huzungumza na waandishi akiwa ametulia na kucheka, safari hii alionekana kufura baada ya timu yake kuwafunga Middlesbrough 2-0 katika michuano ya FA na kuingia robo fainali dhidi ya Manchester United.

Pamekuwapo tetesi kwamba baada ya Pep Guardiola, chaguo la kwanza la Roman Abramovic kuwa kocha Chelsea kwenda Bayern Munich, Benitez ameomba apewe kibarua hicho moja kwa moja, lakini wachezaji na wadau wengine walionesha shaka.

“Nimeongoza soka kwa miaka 26, nimeshinda Kombe la Mabingwa Ulaya, Kombe la Klabu la Dunia, kombe Kombe la FA, Super Cup ya Italia, La Liga Hispania mara mbili – makombe tisa, yaani makombe yote unayoweza kutwaa katika ngazi ya klabu,” ndivyo alivyoanza kufoka Benitez.

“Kundi hili la mashabiki haliisaidii klabu, wanaimba na kupoteza muda kuandaa mabango. Hii ni kwa sababu kuna mtu alifanya kosa hadi ikaandikwa cheo changu ni kocha wa muda, na naondoka mwisho wa msimu, hivyo wasipoteze muda na mimi, wawekeze kuiunga mkono klabu,” akaonya.

Tamko lake hilo halitarajiwi kumpendeza Abramovich, na kwa vile bilionea huyo wa Kirusi hana uvumilivu, si ajabu Benitez asimalize hata huo muda mfupi aliopewa, akitarajia kuwavaa Manchester United Machi 10.

Mashabiki wengi bado wanamlilia Di Matteo, aliyewapa Kombe la Mabingwa Ulaya mara ya kwanza katika historia, lakini Benitez alionya:

“Mimi ndiye kocha na nitaendelea kuiongoza timu. Napenda kuwaongoza wachezaji, si majina, hivyo nitachagua ninaotaka wacheze na kufanya uamuzi wote hadi mwisho wa msimu nitakapoondoka, maana mimi ni wa muda tu,” akahitimisha.

 

Enhanced by Zemanta

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

Tamu na chungu wamiliki wageni klabu za England

Kutoka TFF Leo…