Barcelona wawachapa Bayern 3-0

 

Barcelona wameonesha umwanba wao kwa kuwanyuka Bayern Munich 3-0 katika mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL).

 

Kocha wa zamani wa Barca, Pep Guardiola alikuwa akirudi nyumbani katika timu aliyochezea, kufundisha na kupata nayo mataji, lakini ameduwazwa.

 

Hali ilikuwa shwari mwanzoni, ikitarajiwa kwamba walau wangekwenda suluhu, lakini balaa kwa wageni ilianza kipindi cha pili, kwani kunako dakika za 77 na 80 Messi alionesha ufalme wake, kisha Neymar akamalizia dakika ya mwisho ya mchezo.

 

Hata hivyo ilikuwa mechi ngumu, kwani hadi dakika 13 za mwisho mambo yalikuwa suluhu. Ilikuwa ni mechi muhimu na kali iliyeompeleka Guardiola kwenye klabu aliyochezea na kufundisha na kuwapa mataji mengi, yakiwamo ya Ulaya.

 

Katika nusu fainali nyingine Jumanne wiki hii, Juventus wamewaduwaza mabingwa wa Ulaya – Real Madrid kwa kuwafunga 2-1.

 

Barca wanaoufindishwa na mchezaji wao wa zamani, Luis Enrique aliyecheza na Guardiola hapo walijihisi katika hali nzuri, ambapo pia wanaongoza katika Ligi Kuu ya Hispania, maarufu kama La Liga.

 

Comments