in , , ,

Arsenal waingia kinamna Afrika

Tanzania haimo!

Klabu ya Arsenal yenye wapenzi wengi Afrika, inaingia kwa namna ya biashara Kenya na Uganda, ikiwa na ushirikiano wa kibiashara na Imperial Bank.
Washika Bunduki wa London hao wanaosakata soka Ligi Kuu ya England (EPL), wametangaza kuweka chapa yao katika kadi za benki zitakazosambazwa katika nchi mbili hizo za Afrika Mashariki.
Ushirika huo utakaodumu kwa miaka mitatu ndio wa kwanza mkubwa wa kimataifa kuridhiwa katika masuala ya fedha, na ni endelevu kwa namna ya pekee katika kukuza mapenzi makubwa kwa klabu hiyo barani Afrika.
kadi hizo zitakuwa na vivutio mbalimbali vinavyohusiana na Arsenal wenye makazi yao kaskazini mwa London, vitakavyoelekezwa kwa wateja wa Imperial na washabiki wa Arsenal nchini Kenya na Uganda, kama vile bidhaa zao rasmi na tiketi kwa ajili ya kushuhudia mitanange katika dimba la Emirates.
Ushirikiano huo utaiwezesha klabu pia kuwasogelea karibu zaidi mamilioni ya washabiki wake barani Afrika, huku makocha wa Shule za Soka za Arsenal wakitembelea Kenya na Uganda kama sehemu ya makubaliano ya kuendesha mafunzo ya ukocha na soka kwa niaba ya Imperial Bank.
Shughuli hiyo ya mafunzo itakwenda sambamba na programu nyingine ya Imperial Bank ya kuibua na kukuza vipaji vya soka kuanzia ngazi za chini, lengo likiwa kujenga timu imara za vijana zitakazojumuishwa kwenye mafunzo hayo barabara.
“Tumefurahi sana kuungana na Imperial Bank ili kusambaza kadi za benki zenye chapa ya Arsenal kwa mamilioni ya washabiki Kenya na Uganda. Imperial Bank ni taasisi inayojulikana vyema na kuaminiwa na wateja wake, jamii na wajibu huu inaoonesha umewaweka wadau wake mbele…tunatarajia mafanikio makubwa sana kwenye ushirikiano huu,” anasema Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Arsenal, Vinai Venkatesham.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Imperial Bank, Abdulmalek Janmohamed alisema wana furaha kubwa kuwa na mwelekeo mmoja na Arsenal katika kazi hiyo kwani inainufaisha jamii, kukuza soka na kuimarisha biashara yao kwa pamoja, ikiweka mbele uendelevu wa masuala ya fedha, uadilifu na uhuru.
Anasema Arsenal itaongeza washabiki na benki yake itawafikia wateja wapya ambao hawakutarajiwa kutokana na ushabiki wao kwa Arsenal, nao watawajengea uzoefu wa maana na wenye msaada kiuchumi maishani.

Report

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

What do you think?

71 Points
Upvote Downvote

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Loading…

0

MAAGIZO YA FIFA KUHUSU UCHAGUZI WA TFF

Arsenal waangusha moja moja